Header Ads Widget

DKT.NCHEMBA AELEKEZA SERA YA TAIFA YA UNUNUZI WA UMMA NA UGAVI KUANDALIWA HARAKA

Na,Jusline Marco ;Arusha

Waziri wa Fedha Dkt.Mwigulu Nchemba amemuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya fedha kuhakikisha anaratibu na kusimamia kwa ukaribu sera ya taifa na mkakati wa ununuzi wa umma na ugavi unaandaliwa kwa haraka ili kuhakikisha ununuzi wa umma na ugavi unaofanyika kwenye taasisi za umma unazingatia misingi ya sera hiyo

Dkt.Nchemba ametoa maelekezo hayo Septemba 12 wakati akifunga Jukwaa la 16 la Ununuzi wa Umma Afrika Mashariki lililofanyika kwa siku nne jijini Arusha ambapo amesema kwa kufanya hivyo kutaweza kuweka utaratibu mzuri zaidi wa kusimamia fedha zinazotengwa kwa ajili ya ununuzi wa umma na ugavi kila mwaka

Aidha amesema  serikalk ya awamu ya sita iko mstari wa mbele kuhakikisha kauli mbiu ya Jukwaa la 16 la Ununuzi wa Umma Afrika Mashariki inatekelezwa kwa vitendo kupitia mfumo wa Ununuzi kwa njia ya kielektroniki wa NeST ambao unaleta mapinduzi na uwazi katika sekta hiyo.

"Kupitia sheria mpya ya ununuzi wa umma sura namba 410 ,taasisi zote za umma zinapaswa kufanya hatua zote za ununuzi kupitia mfumo wa NeST kwa lengo la kuhakikisha matakwa ya sheria hiyo yanazingatiwa sambasamba na kuongeza uwazi,uwajibikaji,ushindani na thamani ya fedha zinazotumika katika shughuli hiyo."alisisitiza Dkt.Nchemba

"Ni furaha yangu kuona nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinatekeleza kazi za ununuzi na ugavi kupitia mifumo ya Kielektroniki."Aliongeza Dkt.Nchemba

Ameongeza kuwa Tanzania ipo tayari kushirikiana na nchi nyingine ndani na nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuimarisha matumizi ya ununuzi na ugavi kwa njia ya kidigitali.


Mkurugenzi Mkuu wa PPRA Denis Simba amesema kupitia Kauli mbiu katika Jukwaa la 16 la Ununuzi wa Umma katika Nchi za Afrika Mashariki Tanzania imeonyesha mfano wa kuishi kauli mbiu hiyo kwani tayari imeanza kutumia mfumo wa kidigitali na kuanza kuona faida ya matumizi yake katika ununuzi wa umma kupitia mfumo wa Nest.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Udhibiti wa Umma Kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt.Leonada Rafael Mwagire amesema mada zilizowasilishwa katika mkutano huo zimelenga kuhamasisha matumizi ya Tehama kwenye ununuzi wa umma ili kuweka usawa ,haki, ushindani, uwajibikaji na ufanisi kwenye ununuzi wa umma.


Awali akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda,Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Amir Mkalipa amesema kwa kuipa umuhimu sekta ya ununuzi wa umma maboresho makubwa katika mchakato wa manunuzi yameonekana ambapo ameahidi kuwa uongozi wa mkoa wa Arusha utasimamia matumizi sahihi ya mfumo wa Nest.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI