Na Fredy Mgunda ,Nachingwea.
MKUU wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amewataka watendaji wa vijiji na kata kufuata taratibu,kanuni na Sheria za nchi kuongoza katika maeneo wanayoyaongoza.
Akizungumza wakati wa kongamano la watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea,Moyo aliwataka watendaji kuacha tabia ya kuburuzwa na wanasiasa kwa ajili ya maslai ya kisiasa ambayo yanapingana na Sheria na katiba ya nchi kama ambavyo inatakiwa kutekelezwa
Moyo alisema kuwa watendaji ndio viongozi wa maendeleo wanaotakiwa kusimamia kila kitu katika maeneo wanayoyaongoza Kwa mujibu wa Sheria na katiba ya nchi inavyotaka
0 Comments