Meli ya MT Sangara inavyoonekana sasa baada ya ukarabati mkubwa
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Meli ya Mafuta ya MT Sangara iliyokuwa katika ukarabati mkubwa imefanyiwa ukaguzi na majaribio ya mwisho ya mitambo yake ikiwa katika asilimia 96% kabla ya kukamilika na kukabidhiwa serikalini ili kuanza kazi zake katika Ziwa Tanganyika.
Meli hiyo yenye uwezo wa kubeba tani 380 sawa na lita 410,000 za mafuta ilisimama kufanya kazi tangu Octoba mwaka 2020 kutokana na uchakavu wa mitambo ya Injini jambo lililoathiri usafirishaji wa mafuta ana hivyo serikali kuamua kutoa fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 8.4 ili kuifanyia ukarabati mkubwa.
Mhandisi wa Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania MSCL ambaye ni Msimamizi wa Mradi wa Meli ya MT Sangara, Mhandisi David Jenga, akitoa maelezo kwaa wataalam wa wizara ya uchukuzi waliokuwa wakiifanyia ukaguzi wa mwisho na majaribio alisema kuwa ukarabati mkubwa uliofanywa utawezesha ufanisi mkubwa wa utendaji kazi wa meli hiyo.
Meli ya MT Sangara inatoa huduma ya kusafirisha mafuta kutoka Bandari ya Kigoma kwenda Bandari za Kalemie na Uvira katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na nchi ya Burundi.
Kaimu manager wa tawi la MSCL Kigoma ndugu Aled Butemelo amesema kukamilika kwa meli hiyo kutatoa auheni kwa wafanya biashara wa mafuta hasa kwa nchi za Congo na Burundi ambapo meli hiyo inafanya safari zake kusafirisha mafuta.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya wataalam wa meli kutoka wizara ya uchukuzi Mhandisi Lukombe King'ombe amesema kuwa baada ya ukaguzi na majaribio watatoa taarifa rasmi ya awali ili kupisha taratibu zingine ziweze kuendelea kuwezesha meli hiyo kuanza kutoa huduma.
Mwisho.
0 Comments