Header Ads Widget

ASKOFU MSTAAFU PROF. MDEGELA AKEMEA MATUKIO YA MAUAJI NA UTEKAJI NCHINI

 



Na Matukio Daima App,


Askofu Mstaafu, wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Prof. Owdenburg Mdegela, amekemea matukio ya kikatili yanayoendelea nchini Ikiwemo mauaji na na utekaji na kutolea mfano nchi ya Kongo namna ambayo imekuwa kwenye machafuko kwa miaka mingi kutokana na mauaji yaliyofanyika miaka iliyopita.


Askofu, Profesa Mdegela ameongeza kuwa siku zote damu ya mwanadamu inatabia ya kudai ama kulia hivyo kuendelea kwa matukio kikatili hapa nchini, kutaliathiri taifa la Tanzania, hivyo ameiomba serikali kuangalia namna ya kuadhibiti matukio hayo ili kurudisha imani ya watanzania kwa vyombo vya usalama.


"Yako mauaji ya aina nyingi mara usikie watoto wameua, mara usikie watoto wamepotea na wamepatikana hawana viungo, mara viongozi fulani wa chama wanakufa kiajabu ajabu, na hapa ninasema kama mtumishi wa Mungu nyie umnaijua Congo ndiyo tajiri kwa nchi zote afrika kwa mali asili, lakini haituli kutokana na damu ya Patrice Lumumba inalia"Alisema Profesa Mdegela.


Nchi ijaribu kutumia mbinu zake kuwawabana hawa wanaosababisha vifo vya wengine bila sababu yoyote pamoja na vyama vya siasa kuachana na fitina za kisisa ili kukomesha haya mauaji.



Aidha, Askofu, Profesa Mdegela amewataka wananchi wa mkoa wa Iringa kujitafari upya ili kuona namna ya kuondokana na matukio mabaya yanayonekana kushamiri zaidi ndani ya mkoa huo.


Amesema mkoa wa Iringa umekuwa na matukio ya kutisha kama vile ubakaji na ulawiti wa watoto, ulevi kupindukia, utapiamlo, kukithiri kwa imani za kishirikina pamoja na kuwa kinara katika maambukizi ya ukimwi jambo ambalo halileti taswira nzuri.


"Ninafikiria hata kuomba kibali cha serikali ili kupata nafasi ya kuzungumza mkoa kwa mkoa na hapa Iringa nitasemea Samora ili kukemea mambo haya ambayo yanatia kinyaa, kwani kila siku tunasikia matukio ya kutisha na mengine yakifanywa na tuliotegemea watulinde, kwani damu hii inayolia ikiendelea itatugusa hata tusi husika" alisema.


Pia, amewakumbusha viongozi wanaoteuliwa kuwa na busara katika uzungumzaji wao ili kujiepusha na uzuaji wa taharuki kwa jamii inayowaongoza.


"Mtumishi anayeteuliwa anapaswa kujua namna ya kutunza siri na ndiyo maana wanakula viapo" Alisema.


Katika hatua nyingine, Askofu, Profesa Mdegela, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassani, kutokana na utendaji wake kuwa bora, na kuongeza kuwa anajua kuna watu watamkosa ila kwa umri wake ameona marais wengi wa Afrika na utendaji wao, hivyo anavyompongeza anatambua anachokisema.


"Mimi nimeangali viongozi wengi wa Afrika ila Rais Samia bado ni kiongozi mzuri sana najua watu wanasema anapewa pesa na waarabu siju nini sasa vitu kama hivi ulikuwa wapi wakati anapo pewa pesa hizo"Alisema.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI