WATU kadhaa wanadaiwa kufariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa na wengine wakiwa mahututi kufuatia ajali ya basi lenye namba za usajili T 282 CXT mali ya Kampuni ya AN ambayo hufanya safari zake kati ya Mbeya Tabora .
Ajali hiyo inadaiwa kutokea eneo la Lwanjoro Wilaya ya Mbeya vijijini ambapo Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Chunya Dr.Darson Andrew amethibitisha kuwapokea Majeruhi na maiti 11 kati yao Wanaume watano na Wanawake sita.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.
0 Comments