Header Ads Widget

YANGA SC BINGWA NGAO YA JAMII 2024



Na: Dickson Bisare Matukio Daima Media App -Dar Es salaam.


Timu ya Dar es salaam Young Africans Maarufu kama Yanga Sc wameibuka mabingwa wa Michuano ya Ngao ya Jamii 2024.

Yanga Sc ambao wamekuwa na mchezo wao wa Fainali dhidi ya Timu ya Azam Fc mchezo ambao umechezwa Leo katika uwanja wa Benjamin Mkapa Stadium jijini Dar es salaam na kuweza kuibuka mshindi Kwa magoli manne ambayo yamefungwa na wachezaji wafuatao Stephanie Aziz Ki, Clement Mzize, Prince Dube na Yoro Diaby (OG).

Kwa idadi ya magoli hayo yameweza kuipeleka timu hiyo kuwa Bingwa wa Ngao ya Jamii Kwa mwaka 2024 ambapo pia ni mchezo wa ufunguzi wa msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara  NBCPL 2024/2025.

Nayo timu ya matajiri wa Dar es salaam Azam Fc wamemaliza kama  mshindi wa pili katika Michuano hiyo ya Ngao ya Jamii Kwa mwaka wa 2024 baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Yanga SC Kwa kukubali magoli manne (4) Kwa goli moja.

Nao watani wao jadi Simba Sc wameibuka kuwa mshindi wa tatu katika Michuano ya Ngao ya Jamii 2024 baada ya mchezo wao wa Kwanza ulionza Majira ya saa 9:00 kamili alasiri katika uwanja wa Benjamin Mkapa Stadium dhidi ya timu ya Coastal Union kutoka mkoa wa Tanga na kupanda bao moja ambalo lilifungwa na mchezaji Saleh Karabaka katika dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI