Header Ads Widget

BREAKING:TUNDU LISSU NA WENZAKE WAKAMATWA NA POLISI MBEYA



JESHI la polisi mkoani Mbeya limewakamata  viongozi wakuu wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo ( CHADEMA) wakiongozwa na makamu mwenyekiti Taifa Tundu Lissu ambao walikuwa ndani ya ofisi za CHADEMA Kanda ya Nyasa wakiendelea na kikao Cha ndani .

Taarifa ambazo Matukio Daima media imezipata kuwa viongozi hao walifika mkoani Mbeya Kwa ajili ya  kuadhimisha siku ya Vijana inayofanyika Kitaifa kwa Chama hicho Jijini Mbeya .m

Msemaji wa chama Jon Mrema amewataka viongozi waliokamatwa usiku huu mbali ya Lissu wengine  Katibu mkuu John Mnyika, Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi na viongozi wa Baraza la Vijana (BAVICHA) Vitus Nkuna ambae ni Mwenyekiti BAVICHA Kanda ya Nyasa.

Kamata mata ya wafuasi hao wa CHADEMA ni kutokana na agizo la Kitaifa la Jeshi la polisi kupiga marufuku mikusanyiko ya kisiasa kwa chadema kuwa inaviashiria vya Kuvuruga amani ya nchi.

FULL VIDEO YA CHADEMA KUKAMATWA INGIA CHANEL YA MATUKIO DAIMA TV 

TAZAMA VIDEO BOFYA LINK HII

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI