Header Ads Widget

UVCCM NA DHAMIRA YA KUUNGA MKONO MATUMIZI YA NISHATI SAFI.

 


Na WILLIAM PAUL.


KATIKA Dunia ya leo, ambapo maendeleo ya jamii yanategemea matumizi ya teknolojia na nishati safi, ni muhimu sana kwa vijana kupewa kipaumbele kama nguzo kuu ya mustakabali wa taifa letu. 


UVCCM, kama jumuiya yenye dhamana ya vijana wa Kitanzania, inaendelea kutimiza wajibu wake  katika kuhakikisha vijana wanakuwa sehemu ya mabadiliko haya kwa maendeleo ya taifa .



Nelson Mandela aliwahi kusema, *"The youth are the backbone of any nation. Empower them, and you empower the future."* Hii inamaanisha kwamba vijana ndio uti wa mgongo wa taifa lolote; ukiwawezesha na kuwapa nguvu, unakuwa umeuwezesha mustakabali wa Taifa hilo.


Kwa hiyo, UVCCM kama jumuiya ya vijana wa Kitanzania, tunatambua kuwa mustakabali wa Taifa letu upo mikoni mwetu. 



Tunatekeleza wajibu wetu wa kuwawezesha vijana  ili waweze kuchangia ipasavyo katika maendeleo ya taifa letu.


Mohammed Ally Kawaida, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, kwa kushirikiana na viongozi wenzake wa UVCCM, wamekabidhi mitungi mia mbili (200) ya gesi kwa Wajumbe wa Baraza la UVCCM kwa Mikoa yote ya Unguja. 



Hii ni hatua muhimu katika kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar Dkt.Huseein Ali Mwinyi , katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.


Matumizi ya nishati safi ya gesi yana umuhimu mkubwa katika kuimarisha maisha yetu vijana na maendeleo ya taifa letu kwa ujumla.



 Kupitia teknolojia hii, wanajenga misingi ya mazingira safi, afya bora, na maendeleo endelevu.


 Nishati safi inachangia kupunguza athari za mabadiliko ya tabia ya nchi na kuunda fursa za kiuchumi, hivyo kuimarisha mustakabali wa kijamii na kiuchumi wa leo na kesho.


Aidha pia, aliwasisitiza viongozi kudumisha umoja na mshikamano kwa maslahi mapana ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na maendeleo ya taifa kwa ujumla. 


Jukumu la UVCCM ni kuhakikisha vijana wa Kitanzania wanapata nyenzo muhimu zinazowawezesha kuwa viongozi bora na raia wa mfano, ili kujenga Tanzania yenye maendeleo.


Kugawa mitungi ya gesi ni hatua muhimu sana katika kuwapa vijana nishati safi, ambayo itawasaidia katika shughuli zao za kila siku na kuboresha maisha yao. 


UVCCM inawaalika wadau mbalimbali kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt. Samia kwa kutoa msaada na rasilimali kwa vijana ambapo ushirikiano wao utasaidia kuimarisha mustakabali wa Taifa kukuza maendeleo endelevu, na kuhakikisha kwamba vijana wanachangia kwa nguvu katika ujenzi wa Tanzania yenye mafanikio.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI