Mkuu wa mkoa wa Rukwa Charles Makongoro Nyerere agosti 17,2024 amefungua Ziwa Tanganyika Katika ukanda wa mkoa wa Rukwa akimwakilisha waziri wa mifugo na uvuvi Mh Abdalah Hamis Ulega huku akieleza lengo la kupumzisha ziwa hilo ikiwa ni uamuzi wa utekelezaji wa mkataba wa kikanda wa nchi wanachama wa mamlaka ya ziwa Tanganyika (LTA) unaoweka hatua za usimamizi wa uvuvi endelevu katika ziwa Tanganyika na bonde lake.
Hatahivyo wawakilishi wa wavuvi Wameeleza hayo wakati wa Hafla ufunguzi ya Ufunguzi wa Ziwa Tanganyika katika kijiji cha kasanga baada ya kufungwa kwa kipindi cha miezi 3 huku wakisema wameunga mkono mpango huo wa serikali wa kupumzisha shughuli za uvuvi kwa muda kwani umesaidia kuongeza mazao ya uvuvi kutokana na samaki na dagaa kuonekana kwa wingi hata kabla uvuvi haujaanza.
Akizungumza katika zoezi hilo Naibu katibu mkuu wizara ya mifugo na uvuvi,Dr Edwin Mhende amesema kuwa uvuvi imekuwa moja ya sekta kuu ya uchumi nchini ikiajiri watanzania zaidi ya Milioni sita sawa na asilimia 10 ya watanzania ikiwa kipindi cha miaka 10 vyombo vya uvuvi vimeongezeka kwa asilimia 7 kukiwa na mialo 104 ambavyo vinahudumia rasilimali za uvuvi katika ziwa Tanganyika.
Kupumzishwa kwa shughuli za ziwa Tanganyika zilianza mnamo mei 15 hadi agosti 15 mwaka 2024 yakiwa ni makubaliano ya kimkataba baina ya nchi zinazotumia ziwa Tanganyika zikiwemo Zambia, Ruwanda, Burundi, Kongo na Tanzania ili kuruhusu samaki na viumbe wengine wa majini wazaliane kwa wingi na kukua na kuwezesha rasilimali za uvuvi kunufaisha idadi kubwa ya wananchi.
0 Comments