Header Ads Widget

DC SAME "HATUTAKI VIONGOZI WANAOSHINIKIZA KUCHAGULIWA KWA MISINGI YA RUSHWA”



NA WILLIUM PAUL, SAME. 


MKUU wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni amewataka wananchi kutowachagua viongozi wanaoshinikiza kwa kutoa Rushwa. 



Mgeni alitoa kauli hiyo alipofanya mkutano wa hadhara wa wananchi wa kijiji cha Kavambughu kata ya Same ambapo alisema kuwa kiongozi bora hawezi kuchaguliwa kwa kutoa Rushwa. 


“Kama isemavyo kaulimbiu ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 Tanzania bara.. Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki.. niwaombe Wananchi wa Same kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kugombea na kuchagua viongozi ambao watawaongoza kwa kipindi cha miaka mitano mingine”. Alisema Kasilda. 



Ametoa wito kwa Wananchi wa Same kujianda kuchagua viongozi waadilifu, viongozi bora na sio bora viongozi, na kusisitiza kuwa uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa muhimu sana na ndiyo unaotoa dira ya uchaguzi mkuu wa 2025 wa Rais, Wabunge na Madiwani.


“Chama cha Mapinduzi na mimi Mkuu wenu wa Wilaya hatutaki viongozi wanaoshinikiza kuchaguliwa kwa misingi ya rushwa, viongozi wa namna hiyo hawatufai achaneni nao kabisa”. Alisema. 



Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 Tanzania bara utafanyika November 27, kampeni kwa wagombea wa vyama vyote vya siasa vitakavyoingia kwenye kinyang’anyiro hicho zitafanyika siku saba kabla ya tarehe na siku ya uchaguzi, huku zoezi la upigaji kura litaanzai saa mbili kamili asubuhi na kukamilika saa kumi kamili jioni.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI