Header Ads Widget

TPA : HAKUNA UPOTEVU WA MAPATO BANDARI YA KIGOMA



Na Fadhili Abdallah,Kigoma 


Mamlaka ya usimamizi wa bandari (TPA) imesema kuwa hakuna upotevu wa mapato unaotokea katika bandari ya Kigoma na kwamba tozo na makusanyo yote ya kisheria yamekuwa yakikusanywa kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo kwenye bandari hiyo.


Meneja wa bandari za ziwa Tanganyika Edward Mabula alisema hayo akieleza kuhusu kauli ya baadhi ya wafanyabiashara wa mkoa Kigoma kwamba  ukusanyaji mbaya wa tozo ya  wanaotozwa abiria wanaosafiri nje ya nchi (EMBARKED) Maarufu kama tozo ya udongo umekuwa ukisababisha kupoteza mapato.



Mabula alisema kuwa tozo hiyo ipo kihalali ikikusanywa na Mawakala wa meli kwa niaba ya Mamlaka ya Mamlaka ya Mapato (TRA) kupitia tiketi za kusafiria na kwamba hakuna abiria anayesafiri nje ya nchi kupitia bandari hiyo ambayo anasafiri bila tiketi.


Akizungumzia ajenda iliyoibua jambo hilo kwenye kikao cha baraza la biashara alisema kuwa ajenda ilitaka tozo hiyo ya dola 10 Embarked  iondolewe kwani imekuwa kero kwa abiria na kwamba ufafanuzi wa mamlaka zinazohusika zilitoa ufafanuzi wa pamoja.


Kwa upande wake Mamlaka ya Mapato (TRA) imesema kuwa ndiyo inahusika na ukusanyaji wa tozo ya abiria wanaosafiri nje (Embarked) au tozo ya udongo na inakusanywa na wakala wa meli kwa niaba ya TRA.



Meneja wa TRA mkoa Kigoma,Deogratous Shuma alisema kuwa   tozo hiyo inakusanywa kwa mujibu wa sheria ya Huduma za bandari kifungu cha 264 ambapo kila abiria anatozwa dola tano na inakusanywa na wakala wa meli kwa niaba ya TRA.


Katika azimio ya baraza la biashara kuhusu kodi hiyo na kodi nyingine baraza limeshauri kodi hizo zikusanywe sehemu moja kutoka mamlaka mbalimbali katika bandari za Kigoma kuepuka usumbufu na upotevu wa mapato jambo ambalo TPA na TRA wameshaanza vikao kuzungumzia maazimio hayo.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI