IRUWASA inawataarifu wateja wake kuwa Hali ya umeme Ndiuka sio nzuri. Umeme ni mdogo (Low Voltage)
Hali hii imetokea tangu saa 8 usiku hadi sasa. Uzalishaji wa maji umesimama ili kupisha wataalamu wa TANESCO kurekebisha tatizo.
Kufuatia Hali hii, Maeneo mengi ya Mji wetu yameanza kukosa maji.
Tunawaomba wateja wetu kuwa wavimilivu wakati wenzetu wa TANESCO wakitatua changamoto ya umeme
IRUWASA inawaomba radhi wateja wake kwa usumbufu uliojitokeza.
Muda wowote matengenezo yakikamilika uzalishaji wa maji utaanza na huduma itarejea kama kawaida.
0 Comments