Header Ads Widget

DC DR SELEKWA AENDESHA KIKAO CHA DCC MUFINDI "WADAU WAFUNGUKA ELIMU NCHINI ISICHEZEWE".

Dr.Linda Salekwa - Mkuu wa Wilaya ya Mufindi na Mwenyekiti wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya ( DCC) akifafanua jambo katika kikao .

Na Fredrick Siwale -Matukio Daima APP - Mufindi.

WADAU wa Sekta ya Elimu Mufindi wameiomba Serikali kuweka mikakati thabitika kwenye mfumo wa elimu Nchini ili usichezewe na kila mwenye Mamlaka .


Lai hiyo imetolewa na Wadau wa Maendeleo katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya( DCC ) Mufindi mkoani Iringa,kwa kuwakutanisha Viongozi Serikali, Vyama vya Siasa , Viongozi wa Kidini na Wananchi .             


Awali Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Dr.Linda Salekwa ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho ,aliwataka Wadau kuchangia na  kujadili hali ya utekelezaji wa dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa Wadau na Serikali kuendelea kutekeleza mipango ya Maendeleo inayoongozwa na dira ya 2025.  


Dr.Salekwa alisema majadiliano na michango inapaswa kujikita kujadili miaka 20,10 au miaka mitano (5) I'll yopita ya , mafanikio ya Jumla yanayotokana na utekelezaji wa dira ya mipango ya  Taifa ya Maendeleo 2025 katika nyanja za kiuchumi, kijamii, Utawala bora,amani na utulivu.


Dr.Salekwa alisema mafanikio, changamoto na mambo yaliyotekelezwa na kuwekwa bayana ili Jamii iweze kuiona Nchi ya Tanzania katika mkutadha unao onekana kwa vitendo kwa miaka 25 ijayo.


Alisema zaidi ya hapo ikiwa ni pamoja na kuona Mtanzania anaonejanaje kuelekea dira ya Taifa ya 2050.                                     

Bw.Deogratias Lugenge mdau wa Sekta ya Elimu Mufindi alisema Serikali imejitahidi kuboresha miundo mbinu ya Elimu lakini imeshindwa kuelewa na kusahau Wanafunzi wa kidato cha nne na sita baada ya kuhitimu wanakwenda wapi? Alihoji.   


" Tanzania kwenye sekta ya Elimu kuna siku tutajajikuta kuna Waziri anamua kubadili mtaala kwa jinsi aonavyo yeye" Alisema Bw .Lugenge.


" Hivi Tanzania tumewahi kujiuliza Wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne na sita huwa wanakwenda wapi na kufanya nini " Alihoji.


Mfumo wa Maadili ya Kitanzania unaotakiwa kufuatwa na kuzingatia taratibu, kanuni na tamadu za Kitanzania na sio za Kigeni ili kuifikia 2050.


Tabia ya kuiga kila tamaduni za Kigeni na kuziacha za Kitanzania ndivyo kizazi kinavyozidi kupotoka na kusahau na kuige zile za kigeni.


Wengine waliochangia ni pamoja na Bw.Jonas Kitiga na Elisey Ngoi ambao waliiomba Serikali kusimama kidete Katika suala zima la Utamaduni na Utanzania badala ya kukiacha kizazi kilichopo na kijacho kuendelea kukumbatia ukoloni .                          


"Leo hii Nchi nyingine za Ulaya kila Taifa Utamaduni wake na Lugha yake ya Taifa mfano China,Ufaransa ,Ureno , Ujerumani na Marekani na Uingereza Wana lugha ya Taifa lao na Lugha zao za kufundishia na kujifunzia iweje sisi tuendelee kung'ang'ania Kiingereza? Alihoji Bw.Ngoi.

 


Upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mufindi Mhe.George Kavenuke,alisema Watanzania wanapaswa kutambua kuwa Maendeleo hayana Chama hivyo tabia ya kupinga kila jambo la Maendeleo ni kujaribu kufifisha jitihada na juhudi za Serikali.              


Alisema ni muhimu Wadau wanapochangia waondoe dhana ya upinzani na zaidi wazungumzie dira ya mipango ya Taifa ya Maendeleo 2050.                 


" Kama kuna mtu afahamu kuwa Vyama vingi havikuanza leo basi ngoja niwaingize darasani , Maendeleo ya Kisiasa yalianza mwaka 1959 ambapo Utawala wa Waingereza ulianzisha Uchaguzi wa kidemokrasia wa Vyama vingi wa kura 3" Hilo mnalikumbuka ? Alihoji Mhe.Kavenuke.               


Aidha aliongeza kuwa mwaka 1965 vile Vyama vilivunjwa na kubakia Chama kimoja baada ya Uhuru cha TANU na CCM na mwaka 1992 mfumo wa Vyama vingi.                      



Bw.Jonas Kitiga - Katibu wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA )Wilaya ya Mufindi  akisisitiza kuhusu Maadili.



DC Mufindi Dkt Selekwa akisoma taarifa

Baadhi ya washiriki wa kikao Cha kamati ya ushauri wilaya ya Mufindi 




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI