Header Ads Widget

NG'OMBE 27 ZATOLEWA KWA WALENGWA WA TASAF MAKAMBAKO NJOMBE



Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Walengwa wa mradi wa Kunusuru kaya masikini TASAF katika kijiji cha Ikelu Halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe wamewezeshwa kufuga Ng'ombe wa maziwa watakaowasaidia kujinusuru na hali ngumu ya maisha inayowakabili kwa sasa.

Mratibu wa TASAF Halmashauri ya  mji wa Makambako Neema Chaula amesema Ng'ombe hao wametolewa kwa walengwa 27 wa Kitongoji cha Nyambogo kijiji cha Ikelu Mradi ambao wameuibua wananchi wenyewe unaogharimu kiasi cha shilingi milioni 25.



Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka ametembelea na kukabidhi Ng'ombe hao na kwamba hatua hiyo itawafanya kuwa na uchumi mzuri na endelevu badala ya kuwapa fedha ambazo huisha baada ya muda mfupi.

Baadhi ya Walengwa wa TASAF Katika kijiji cha Ikelu akiwemo Inick Kidenya,Christina Mduba na Fausta Mwagike wanakiri kuwa mradi huo utawasaidia kwa ukubwa kwani hata fedha ambazo wamekuwa wakihaulishiwa zimewasaidia kuboresha maisha yao kwa kiasi.



Mussa Seleman ni Mratibu wa Tasaf Mkoa wa Njombe ambaye anawataka wananchi hao kutunza vyema Ng'ombe hao ili waje kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na kwamba atakayeshindwa atapokwa mradi.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa anasema mbali na mradi huo kwenda kuwainua kiuchumi wananchi lakini pia utasaidia kupunguza changamoto ya Udumavu kwa wananchi.

Walengwa wenyewe wa TASAF Wanakiri kusaidika katika maisha yao.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI