Header Ads Widget

MBUNGE ANNE KILANGO AKIRI UCHAGUZI KUWA MGUMU.

 


NA WILLIUM PAUL, DODOMA. 


MBUNGE wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela amesema kuwa uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani ni uchaguzi mgumu kuliko chaguzi zote zilizowahi kufanyika hapa nchini. 


Mbunge Anne ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza na viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Jimbo la Same mashariki nyumbani kwake jijini Dodoma. 



Alisema kuwa, kwa sasa viongozi wa vyama vya upinzani wameanza kupitapita katika Jimbo hilo kuanza kutengeneza watu ambao watawasimamisha kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kuanzia Serikali za mitaa. 


"Natambua Chadema wameanza kuweka kambi katika jimbo letu lakini niwahakikishie hawatapata nafasi hata moja ninachokitaka kwa sasa tushikamane wana ccm kupambana nao" Alisema Anne Kilango.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI