Header Ads Widget

VIONGOZI UVCCM JIMBO LA SAME MASHARIKI WAWASILI DODOMA KWA MWALIKO MAALUM WA MBUNGE ANNE KILANGO.

 


NA WILLIUM PAUL, DODOMA. 


VIONGOZI wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Jimbo la Same mashariki wilayani Same mkoani Kilimanjaro wamewasili jijini Dodoma kwa ajili ya mwaliko wa kushiriki katika kikao cha Bunge kupata uzoefu pamoja na kupata semina maalum ya kuelekea katika uchaguzi wa Serikali za mitaa Novemba mwaka huu. 



Akizungumza mara baada ya kuwapokea viongozi hao ambao ni Wenyeviti wa Kata, Makatibu kata pamoja na Makatibu hamasa kata, Mbunge wa Jimbo la Same mashariki, Anne Kilango Malecela alisema kuwa, lengo la ziara hiyo ni kujifunza mambo mbalimbali ya Chama na Serikali. 



Alisema kuwa, lengo kubwa ambalo wamejiwekea kama Jimbo ni kuhakikisha Chama kinashinda viti vyote ndani ya Jimbo hilo katika uchaguzi wa Serikali za mitaa pamoja na uchaguzi mkuu mwakani. 



"Kesho mtapata fursa ya kuingia Bungeni kuona jinsi shughuli za Bunge zinavyoendeshwa na badae mtapata semina maalum kutoka kwa wakufunzi wa ndani ya Chama ambapo semina hii ni muhimu kwenu katika kuhakikisha kuwa tunashinda kwa kishindo uchaguzi wa Serikali za mitaa" Alisema Anne Kilango.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI