Header Ads Widget

INTER STARS KUPAMBA MASHUJAA DAY

Hamisi Millingo (kulia) Afisa Habari wa timu ya Mashujaa ya mkoani Kigoma inayoshiriki ligi kuu ya NBC
Timu ya Inter Stars ya Burundi itakayoshiriki Tamasha la kutambulisha wacheza wa timu ya Mashujaa FC ya mkoani Kigoma inayoshiriki ligi kuu ya NBC
Afisa Habari wa timu ya mashujaa katika mkutano na waandishi wa habari

xxxxxxxx

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

TIMU ya soka ya Inter Stars inayoshiriki ligi kuu ya nchini Burundi inatarajiwa kupamba tamasha la kutambulisha wachezaji lililoandaliwa na timu ya Ligi kuu ya NBC ya Mashujaa ya mkoani Kigoma kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa ligi hiyo.

 

Tamasha hilo linatarajia kufanyika Jumamosi ya Agosti 10 mwaka huu katika uwanja wa michezo wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma ambapo mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa utakuwa maalum kwa ajili ya kuhitimisha siku hiyo ambayo itatanguliwa na shamra Shamra mbalimbali ikiwemo wasanii.

 

Afisa Habari wa timu ya Mashujaa, Hamisi Ramadhani Millingo akizungumza na waandishi wa Habari kwenye uwanja wa Lake Tanganyika Mjini Kigoma alisema kuwa pia Msanii wa muziki wa Bongo Fleva mzaliwa wa Kigoma Linex Sunday Mjeda atatumbuiza kwenye tamasha hilo.

 

Millingo alisema kuwa katika siku ya Mashujaa  watatambulisha wachezaji 10 waliowasajili msimu huu kuelekea msimu mpya wa ligi na  benchi la  ufundi ikiwa ni matokeo ya maboresho ya kikosi chao kutoka kuachana na wachezaji tisa waliokuwa nao msimu uliopita.

 

Pamoja na mambo mengine alisema kuwa kuelekea tamasha hilo viongozi, wachezaji na wapenzi wa timu hiyo walifanya shughuli mbalimbali ikiwemo kufanya usafi maeneo mbalimbali ya taasisi za umma, kuchangia damu na Ijumaa ya tarehe 9 siku moja kabla ya tamasha hilo walikuwa na ratiba ya kutembelea kituo cha Watoto yatima na kushiriki nao chakula cha mchana.

 

Akizungumzia mkakati wa timu hiyo kwa msimu unaanza hivi karibuni alisema kuwa maboresho ya kikosi chao yamelenga kuifanya timu hiyo kumaliza nafasi nne za juu katika ligi ya NBC baada ya kugundua makosa yaliyafanyika mwaka jana na changamoto zilizojitokeza.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI