Header Ads Widget

HOSPITALI YA SELIAN LUTHERAN NGARAMTONI YAADHIMISHA JUUBILEE YA MIAKA 70

  





Na,Jusline Marco:Arusha

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania Dayosisi ya Magharibi Kati Dkt.Isaac Kisiri Laiser ameupongeza uongozi wa hospitali ya Selian Lutheran Medical Ngaramtoni na Wanadayosisi ya Kaskazini Kati kwa kuendeleza, kutunza na kuyaenzi maono ya waanzilishi wa hospitali hiyo katika miaka 70 iliyopita.



Dkt.Kisiri ametoa pongezi hizo katika Ibada maalum ya Maadhimisho ya Yubilee ya miaka 70 ya hospitali ya Selian Lutheran iliyopo katika eneo la Ngaramtoni Wilayani Arumeru ambapo amesema katika kipindi cha kuwepo kwa hospitali hiyo, imekuwa chombo cha Uinjilisti , Udiakoni na kuhusika kwenye kuleta uponyaji.



Aidha amesema zaidi ya kupongezana kwa Yubilee hiyo ,Mungu awasaidie kuangalia nyuma walikotoka na changamoto zake na kuangalia miaka mingi ijayo zaidi sana Mungu awasaidie waendelee kuwa mawakili wema kwake na kwajamii ambayo wanaitumikia.



Akifafanyua andiko alilolisoma katika Yubilee hiyo kutoka kwenye biblia kitabu cha Yeremia 30:17 Dkt.Kisiri amesema ujumbe huo umelenga kufunua na kueleza mpango wa Mungu wa kufanya mambo mapya,kujenga tena kwa upya na kufanya urejesho ambapo amesema ili hayo yote yawezekufanyika lazima kutanguliwe kwa kuondoa kile kilichokuwepo kilichoharibika.



Dkt.Kisiri amesisitiza jamii kuacha tabia ya uvivu katika kumuomba Mungu na kukimbilia kudanganywa kwenye maombi mbalimbali wakotegemea kufanikiwa pasipo kufanya kazi,badala yake watambue kuwa Mungu ametoa neema ya kwenda kwake kwa njia ya maombia ili mtu akisikia kishindwa na kuishiwa nguvu yeye apate kuwainua, kuwaponya na kuwapa nguvu ya kuendelea kutangaza matumaini kwa waliovunjika moyo na kuuhishwa kwa maisha ya wale wote waliopata vidonda vya kimwili na kiroho.



Akiingiza kazini Bodi ya Hospitali hiyo Mhe.Baba Askofu Dkt.Godson Abel Mollel Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini Kati ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ameitaka bodi hiyo kutimiza wajibu wao kwa ari,uadilifu,uwazi,upendo bila kumuonea mtu yeyote kwa kweli ya Neno la Mungu.



Awali akisoma historia ya hospitali hiyo Mkurugenzi wa Hospitali ua Selian Lutheran Dkt.Amon Marti amesema tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo kwa huduma za afya katika Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kaskazini Kati ambapo amesema ilianza kwa wazo la kuwa Zahanati katika Ukanda wa Maasai mwaka 1952  na kujengwa na wananchi wa Selian wakishirikiana na wanafunzi  wa shule ya msingi Selian.



Ameongea kuwa huduma za afya zilianza kutolewa mwaka 1954 chini ya usimamizi wa tabibu Eliapenda Swai ambapo Idara ya afya katika Sinodi Mkoani Arusha ilianzishwa mwaka 1973 na kuanzisha zahanati mbalimbali zilizokuwa zikisimamiwa na zahanati ya Selian.



Dkt.Marti amesema katika kuadhimisha miaka 70 ya huduma za afya Selian wanakumbuka mchango wa maafisa tabibu, famasia na wauguzi waliosimamia zahanati hiyo kwa ufanisi mkubwa katika kukuza huduma za afya kwenye maeneo ya kifugaji.



Akitaja baadhi ya miradi iliyosimamiwa na hospitali ya Aelian Dkt.Marti amesema ni pamoja na Mradi wa South Maasai Mobile Unit, North Maasai Mobile Unit, Mpango wa kudhibiti Ukimwi, Mradi wa Tiba Shufaa, Mradi wa Fistula, Mradi wa Upasuaji Mifupa, Mradi wa Upasuaji wa mdomo sungura, makovu ya moto na kurekebish majeraha, Mradi wa Maji Safi Loiainoni, Mradi wa Lishe kwa Watoto wenye Utapiamlo, Mradi wa Morechils Surgery na Miradi ya kuwahudumia watu wenye ulemavu.



Tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo zaidi ya wafanyakazi 700 wameajiriwa ambapo kwa sasa kuna wastani wa wafanyakazi 250 na kuendelezwa kielimu na kupata ufadhili wa masomo kwa kada mbalimbali huku katika huduma za afya hospitali hiyo imeweza kuwahudumia wagonjwa zaidi ya milioni mbili na kutoa huduma za madaktari bingwa katika fani za Tiba, Watoto, Afya ya magonjwa ya akina mama, Upasuaji Mazoezi ya viungo, maabara, X-ray, CT-Scan, Utrasound, Huduma za dawa, ICU na NICU, Huduma za wagonjwa wa nje na Kliniki za Madaktari Bingwa, Huduma za kinywa na meno pamoja na Tiba shufaa.



Yubilee hiyo ilienda sambamba na uzinduzi wa vifaa ikiwemo mashine ya kisasa ya X-ray yenye uwezo mkubwa ambayo itasaidia wataalam kupiga na kusoma picha na kuona iliyo sahihi  CT-SCAN ya kisasa ambayo nayo ina uwezo wa kuona mahonjwa kwa upana zaidi pamoja na mashine ya C-ARM ya kisasa ya x-ray  yenye uwezo mkubaa wa kuonesha zaidi ambayo itamsaidia daktari bingwa wa mifupa kuona kiungo kilichotenguka.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI