Header Ads Widget

ZIARA YA MBUNGE WA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI PROFESA PATRICK NDAKIDEMI KATIKA KATA YA OKAONI YATIA FORA

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI. 


Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi na Diwani wa Kata ya Okaoni, Moris Makoi ,  wameshiriki katika ziara ya kikazi katika Kata ya Kibosho Okaoni ambayo ilihudhuriwa na umati mkubwa wa watu .



Ziara hiyo ilimshirikisha Katibu wa CCM Wilaya, Ramadhani Mahanyu, viongozi wa CCM Kata na Serikali kutoka Okaoni na mamia ya wananchi. 



Ziara hiyo ililenga kuwapa wananchi mrejesho wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kwa kipindi cha miaka minne katika Kata ya Okaoni, pamoja na kuwapa miche bora ya migomba.



Akiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya Sekondari Okaoni, Ndakidemi aliwaambia wananchi Kata ya Kibosho Okaoni ilikuwa imepokea miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 1,767,691,308.00. 



Akipokea kero za wananchi, kero kubwa iliyotawala ilikuwa ni ya ubovu wa mifereji ya asili huku kero nyingine ilikuwa ni pamoja na kumaliza ujenzi wa barabara ya International School kuelekea kwa Rafaeli kwa kiwango cha Lami.



Kero ya miradi ya maji ya RUWASA ambayo inatekelezwa katika Kata hiyo bila kuwapa elimu wananchi ambapo Mbunge aliwaambia wananchi kwamba amezibeba kero zote, na atazipeleka kwenye mamlaka husika.



Akiongea katika mkutano huo, Katibu wa CCM Wilaya, Ramadhani Mahanyu amewataka Watanzania kuiunga mkono serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwani amefanya mambo makubwa ya maendeleo. 


Mwisho...

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI