Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App Dodoma
WAZIRI wa Kilimo Hussein Bashe anatarajiwa kufungua mkutano wa 27 wa Wanahisa wa benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (KCBL) na wanahisa wengine walionunua hisa katika benki hiyo.
Kutokana na hayo Wanahisa hao wanaombwa kufika Katika mkutano huo utakaofanyika jijini kesho Julai 26,2024 Dodoma kwa lengo la kutoa taarifa kwa Wanahisa hao kuhusu utekelezaji wa benki na kujua yajayo kwa mwaka unaofuata.
Akiongea leo na waandishi wa habari Julai 25 2024 Mwenyekiti wa Benki ya Ushirika ya Kilimanjaro Prof.Gervas Machimu amewataka wanahisa hao kufika Mkutano huo mkuu wa 27 utakaofanyika jijini Dodoma Julai 26 2024 .
Mwenyekiti huyo amesema,"katika mkutano mkuu huo kazi kubwa ni kwenda kueleza na kuwapa majibu wanahisa kwa yale yote walioagizwa na kueleza Yale wanayotarajia kuyafanya kwa mwaka unaofuata, "ameeleza.
Amesema mkutano huo unafanyika kwa Mara ya kwanza Dodoma na ni wakihistoria kwani ni wa mwisho wa benki ya KCBL na sasa wanakwenda kuanzisha benki ya Ushirika ya kitaifa ambayo inauganisha benki mbili KCBL na benki iliyokuwa yatakoba.
" Wanahisa karibuni katika mkutano huu, wana Ushirika, waluonunua hisa binafsi makampuni, " Amesema.
Meneja Mkuu wa Benki ya Ushirika ya Kilimanjaro Godfrey Ng'urah amesema mkuano Mkuu wa 27 wa wanahisa wa wa Benki hiyo amesema kuwa baada ya miaka mitatu yamchakato wa mageuzi wanaushirika watafanya mkutano wao kwa Mara ya kwanza baada ya mageuzi.
Ajenda mahususi ni pamoja na utendaji kazi wao wa mwaka jana 2023 uliokuwa na mafanikio makubwa katika utendaji lakini pia mkutano huo utaonyesha safari yao ya miaka 3 ya mageuzi.
"Kama walivyotuagiza kwenye mkutano Mkuu wa mwaka uliopita na kuipa bodi mamlaka ya kukamilisha safari hiyo ya mageuzi kuwa Benki ya ushirika Tanzania.
Amesema wanahisa wanayofursa na nafasi kupata matokeo ya kazi kubwa iliofanywa na bodi kwa kushiriana na Menejimeti kuifanya benki ya Ushirika ya Kilimanjaro Katika mageuzi yote kwa kushirikiana na benki ya Ushirika ya Tamdaimba kuwa na benki moja ya Ushirika Tanzania, pili kuwa na matokeo ya kiutendaji Shughuli mbalimbali za kibiashara, bidhaa, huduma za kifedha huko tumefanikiwa kwa kipindi cha miaka mitatu.
Undeshaji wa mifumo utawala bora usimizi na tija uliotokana na Shughuli na uongozi wa 2023 na wanahisa kupitisha maazimio mbalimbali ikiwemo hatua za mwisho za kurasimisha Benki ya Ushirika Tanzania.
" Moja yamaazimio makubwa Katika kipindi cha miaka mitatu 2021mpaka 2023 ni kuhamisha makao makuu kutoka Kilimanjaro kuja Dodoma na mpaka mwezi wa 9 mwana huu litakuwa limekamilika.
Mwishoo
0 Comments