Header Ads Widget

ZAIDI YA MILIONI 11 ZAPATIKANA HARAMBEE UJENZI WA KANISA KKKT IGAGALA NJOMBE

 






Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Zaidi ya shilingi milioni 11 zikiwa fedha taslimu na Ahadi zimepatikana kwa ajili ya ujenzi wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Usharika wa Igagala kata ya Ulembwe wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe katika ibada ya shukrani ya Diwani wa Kata hiyo Agnetha Mpangile mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo kwa kumponya na changamoto yake ya saratani ya mguu.


Mpangile ambaye alikatwa mguu kutokana na changamoto hiyo ameona umuhimu wa kufanya Ibada ya Shukrani katika kata yake ya Ulembwe huko Igagala ambako ujenzi wa kanisa hilo unaendelea uliomfanya kuweka changizo kwa ajili ya kuweka malumalu baada ya kuponywa na mwenyezi mungu.


Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amepongeza hatua ya Diwani huyo kufanya Ibada ya shukrani kwani wapo ambao wanapitia magumu zaidi na hawamshukuru mungu.


Naye Mbunge wa Jimbo la Wanging'ombe na Naibu waziri TAMISEMI Dokta Festo Dugange anasema uamuzi wa Agnetha unafaa kuigwa na Watanzania wanaopitia changamoto mbalimbali zikiwemo za kiafya.


Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Ulembwe na wahitaji mbalimbali  wamesema jamii inapaswa kuwashika mkono watu wanaopatwa na changamoto ngumu kwani hali zao zimekuwa mashakani.


Kwa upande wao baadhi ya wadau wa maendeleo wilayani Wanging'ombe akiwemo Eliud Nyauhenga na Enock Kiswaga ambao walialikwa katika ibada hiyo wamesema suala la ugonjwa halina mwenyewe na hivyo ni muhimu kuwashika mkono wanaopitia changamoto kama alizopitia Mpangile.


Agnetha mbali na kusaidia kupatikana kwa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa kanisa lakini pia naye amewashika mkono baadhi ya watu wanaopitia changamoto za kiafya kwa kuwanunulia viti mwendo pamoja na kuahidi kuwanunulia miguu ya bandia ambayo hata yeye anatumia.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI