Header Ads Widget

ZAIDI YA BIL.150 ZAPELEKWA LINDI KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO

 


Mkoa wa Lindi umepokea zaidi ya Bilioni 150.183 katika kipindi cha mwaka 2023/24 kwa ajiri ya utekelezaji wa shughuli za miradi ya maendeleo katika sekta za Elimu,Afya, Umeme, Miundombinu, Kilimo, Mawasiliano, Madini na Uwekezaji.


Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack wakati akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kipindi cha Novemba 2023- June 2024 ambapo ameeleza kuwa fedha hizo zimechangia kuleta maendeleo kwa kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma kwa wananchi hususani katika sekta ya Elimu na Afya.


"Katika sekta ya Elimu tumepokea Bilioni 36.6 zilizotumika kujenga,kukarabati, kuhifadhi na kuendeleza mazingira ya shule. Aidha, Mkoa umeweza kupokea jumla ya fedha Bilioni 1.768 kwa ajiri ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 71, matundu ya vyoo 182 na mabweni 3 kwa ajiri ya shule ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu. Vilevile, Milioni 974.082 zimepelekwa katika Halmashauri za Wilaya za Nachingwea, Liwale na Kilwa kwa ajiri ya ujenzi wa Vyuo vya VETA" Mhe. Telack.


Mkuu wa Mkoa amewapongeza Maafisa Elimu, Walimu, Wadau wa Elimu, Wazazi na Wanafunzi kwa juhudi zao zinazopelekea kuongezeka kwa hali ya ufaulu ambapo Mkoa umefanikiwa kufaulisha wanafunzi wa kidato cha sita kwa 100% miaka mitano mfululizo na kidato cha nne umefaulu umepanda hadi 95.20% hivyo kupelekea Mkoa kutunukiwa cheti cha kuongeza ufaulu (KPIs) na wizara ya OR- TAMISEMI.


"Katika Sekta ya Afya Mkoa umepokea Bilioni 7.44 kwa ajiri ya ujenzi,ukarabati na ununuzi wa vifaa tiba na hali ya upatikanaji wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya ikiwa ni 93.3%. Aidha, Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa (NHIF) umefanikiwa kufanya malipo ya Bilioni 1.939 katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa ajiri ya kununulia madawa na vifaa tiba. Changamoto ambayo tunaendelea kupambana nayo ni idadi ya wanachama wanaojiunga na mfuko wa afya ya jamii (iCHF) ambapo hadi sasa kaya 3182 sawa na 14% kwa Mkoa mzima wamejiandikisha" ameelezea Mkuu wa Mkoa.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI