Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Jumla ya simu 22 zimekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Njombe kwa watu mbalimbali waliojihusisha na vitendo vya kuvunja na kuiba katika kipindi cha mwezi juni mwaka huu.
Simu hizo zimekamatwa baada ya kufanyika kwa misako mbalimbali iliyofanikisha kukamatwa kwa watu 127 waliojihusisha na wizi huo pamoja na matukio mengine.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga ametoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari na kwamba bado Oparesheni zinaendelea.
Aidha Kamanda Banga amesema Jeshi hilo pia limekamata watu wawili waliohusika katika wizi wa pikipiki ambayo ni Mali ya Halmashauri ya mji wa Makambako huku likiwaonya madereva wanaoendelea kuvunja sheria za baranarani.
Rodrick Mwaigalagala,Paulo Pastory na Changala Mfungo ni wakazi wa Njombe ambao wanakiri kuwa vitendo vya wizi vimekuwa vikiwarudisha nyuma kimaendeleo na vinapaswa kudhibitiwa kikamilifu.
Polisi wametakiwa kuongeza nguvu katika doria wanazofanya na kuwa karibu na Jamii ili kupata taarifa za wahalifu na uhalifu kiurahisi.
0 Comments