Abate wa Abasia ya Ndanda Christian Temu OSB ametoa taarifa ya kuthibitisha vifo vya watawa watatu wa shirika la Mtakatifu Benedikto Ndanda waliofariki kutokana na ajali ya gari katika Kijiji cha Mtua Longa halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi.
Ajali hiyo imetokea mapema alfajiri ya leo Julai 12,2024 majira ya saa 11:45 na ni baada ya gari dogo waliokuwa wakisafiria lenye namba za usajiri T 139 DZZ kuacha njia na kuanguka kwenye Korongo.
Watawa hao waliokuwa wanatokea Ndanda kuelekea Daresalam wakitokea Ndanda ambako Julai 11,2024 kulifanyika sherehe za nadhiri za muda na za daima.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo waliofariki ni Padre.Comellius Mdoe OSB,Padre Pius Boa OSB,Bruda Bakanja Mkenda OSB.
Aidha,inaelezwa dereva aliyekuwa anaendesha gari hiyo amepata majeraha.
0 Comments