Header Ads Widget

UMAUKI YAHITAJI KIASI CHA SHILINGI MILIONI 6.5 KILIMO CHA MATUNDA

 


CHAMA cha Ushirika cha Umoja wa Wanamazingira na Udhibiti wa Uchimbaji Mchanga Kibaha (UMAUKI) kinahitaji kiasi cha shilingi milioni 6.5 kwa ajili ya mradi wa kilimo cha matunda ya pasheni na papai.


Hayo yalisemwa Mjini Kibaha na Meneja wa chama Hicho Mshamu Hay wakati wa uzinduzi uliofanyika Mwendapole Wilayani hapa na kuwa walianza na upandaji miche hadi kupanda lakini nguvu imewaishia huku wakihitaji kupata uzalishaji mzuri.


Mshamu amesema kuwa chama kimeendelea na shughuli za kudhibiti uharibifu wa Mazingira unaotokana na sababu mbalimbali zikiwemo uchimbaji wa mchanga kiholela, ukataji wa miti hovyo na uharibifu wa vyanzo vya maji.  


"Tulitekeleza mradi wa upandaji wa miti ya kivuli na matunda kuzunguka katika mipaka na katikati mwa eneo la shule ya Msingi Muungano,"amesema Mshamu.


Amesema kuwa mradi ambao umekamilika kwa 100 na sasa watoto wetu wananufaika na uwepo wa miti hiyo tumeendelea kufanva kazi mbalimbali rafiki wa mazingira hadi kufikia sasa,"Mshamu.


Aidha amesema kuwa pia wanajihusisha na uvuvi, ufugaji wa nyuki lengo likiwa ni kulinda mazingira ili yawe salama na kurejesha uoto wa asili ambao umetoweka kutokana na uharibufu wa mazingira.


Kwa upande wake Kaimu Ofisa Kilimo Halmashauri ya Mji Kibaha Suzana Mgonja amesema kuwa chama hicho kinapaswa kutumia wataalam wa kilimo ili waweze kuzalisha kwa ubora.

Mgonja amesema kuwa wao wako tayari kushirikiana na wakulima ili kuhakikisha wanainuka na kulima kilimo bora na chenye manufaa siyo kilimo kisicho na tija.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI