Header Ads Widget

UKATILI WA KIJINSIA MUFINDI WANAWAKE , WANAUME WATUPIWA BOMU.

 



Na Fredrick Siwale -Matukio Daima APP - Mufindi.                               

WANAWAKE NA WANAUME Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi mkoani Wametupiwa lawama kufuatia kukithiri kwa vitendo vya Ukatili wa kijinsia kwa Watoto na Wanawake.                        



Akizungumza na Wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Ikongosi Juu ,Mhe.Magreth Kaguo  Diwani wa Viti Maalumu Jimbo la Mufindi Kaskazini,alisema Kuna mahali Wanawake wameshindwa kuzilinda familia zao na kuwaacha watunzwe na kulelewa na Walimwengu.                    


" Wanawake wenzangu wapi tunapo kwamba, Watoto Mimba tubebe sisi tumboni miezi 9 halafu kwenye malezi tuischie Dunia na sisi tutingwe na shughuli za kujitafutia kipato?" Alihoji Mhe.Kaguo.                                


Wakati umefika wakati kwa  Wananchi kurudi kwenye mfumo badala ya kukaa nje ya mfumo , kwani umefika wakati Wanawake wanajikuta kuegemea zaidi  kwenye shughuli za kujitafutia kipato kuliko kutunza na kulea familia.


"Wanawake wenzangu tulipofika sasa Watoto na Waume zetu tumeiachia Dunia itutunzie Ili hali tulibeba ujauzito miezi 9 tumboni mwetu,huu ni uzembe!" Turudi kwenye uhalisia wetu." Alisema Mhe.Kaguo.                           


Alisema kila kukicha tunasikia kuna Mtoto amebakwa , amlawitiwa, ametekwa, amepotea au ameuawa Ili hali Wanaofanya Matukio hayo ni sehemu ya Jamii kwenye eneo husika.


Jeshi la Polisi,Jamii wakiwepo Viongozi wa Kidini na Wazazi umefika muda wa kila mmoja asimame katika zamu na uhalisia wake kuhakikisha matendo haya yanatokomezwa na Wahusika kukamatwa.           


" Wananchi haiwezekani eti Mtoto anabakwa , amlawitiwa, anatekwa, anapotea au anauawa halafu tuseme wahusika hawajulikani ! Huo ni uongo wa mchana kweupe.Aliongeza Mhe.Kaguo.                          


Umefika wakati ambao Wanawake wanapaswa kuwa Walinzi wa kwanza kwa familia zao, Kisha Viongozi wa Kidini, Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Wananchi wote kwa Ujumla.                


Mhe.Kaguo alilaani vikali tabia ya baadhi ya Wanaume wanaofikia hatua za kuwaka tamaa za kingono na kudiriki kuwarudi Watoto wao kwa kuwabaka ,kuwalawiti ama kuwaua bila hatia.     


"Hivi Wanawake wenzangu wapi tunakwama hadi Watoto wetu wanakutwa na madhira haya" ? Alihoji Mhe.Kaguo.                          


Alisema Kuna mahali Wanawake wameshindwa kuzilinda familia zao kwa uzembe au kwa kujali biashara na Kilimo huku Jamii  inaangamia kwa kukosekana kwa hekima na marifa na kwa pamoja kushikamana na kusimama katika uhalisia kulinda kizazi kinachoonekana kukosa Maadili.


Aidha alisema vitendo vya udhalilishaji, Ukatili wa kijinsia, uvunjifu wa haki za Binadamu, Ulawiti,Ubakaji na Mauaji iwapo Watanzania , Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Viongozi wa Kidini mshikamano nguvu ya pamoja vinaweza kukomesha matendo hayo na kuliokoa Taifa na aibu hii.



Katibu wa Jumuiya ya Wazazi (UWT) kata ya Ikongosi Juu Bi.Nelia Chang'a alisema katika Kata yao kumekuwa na Matukio ya ukatili wa kijinsia na ufunzifu wa haki za Watoto yanafanyika lakini hayatolewi taarifa na kuziomba Mamlaka na Wazazi kuacha kuficha vitendo vya uhalifu.                     


Bi.Chang'a alisema vitendo vya udhalilishaji, Ukatili, ubajaji na Ulawiti vikiumbuliwa kwa kutoa taarifa vinaweza kukomeshwa badala ya kuvifanya kuwa siri.


 "Vitendo hivi tunavifuga wenyewe kwa kufichiana siri Ili hali kizazi kipoteza uhalisia wake ,tufunguke na tusemezane na Watoto wetu ili watueleze mambo yanayowasibu majumbani ,Mashuleni na Vyuoni" Alisema Bi.Chang'a.


Kiongozi wa Kidini Mwijilisti Joice Mtokoma wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Mtaa wa Ikongosi Juu aliiomba Jamii kurudi kwenye kuwafundisha Watoto Maadili na kuwashirikisha Viongozi wa Kidini katika maeneo ya kuwafundisha Maadili Watoto na kuomba Mungu awaepushe na Matukio ya sio ya Kimaadili.                                 


Bi.Mtokoma alisema sasa hivi mmomonyoko wa maadili umeshika kasi na kuifanya Dunia ionekane si sehemu salama kwa Watoto na Wanawake, Wanaume na Wazee .

 

Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikongosi Juu,Bw.Amriy  Kidumange upande wake alisema Mufindi inatakiwa kuwa salama kwa Jamii kujilinda na kwa kuzishirikisha Mamlaka kuanzia ngazi ya Kijiji, Mtaa, Kata Wilaya hadi Mkoa.                       


Wananchi tusaidiane kuwafichua hawa Watu wanao tukosesha amani na usingizi kwa ajili ya masuala yao binafsi ya Ubakaji , Ulawiti na Mauaji ya Wazee na Albino.                                     


Wimbo ni mmoja tu " Tokomeza ukatili wa kijinsia, uvunjifu wa haki za Binadamu Watoto na Binadamu na kila mmoja awe mlinzi wa mwingine maana Wahalifu tunaishi nao tuwaseme wazi na kwa siri. Alisema Kidumage.                          


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI