Header Ads Widget

MELI VITA TATU ZA JESHI LA UKOMBOZI WA CHINA ZATIA NANGA NCHINI

 


Na Matuo Daima Media, Dar es Salaam

MELI Vita tatu za Jeshi la Ukombozi la watu wa China zimepokelewa nchini jana kwa ajili ya kuungana na vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika mazoezi ya miaka 60 ya ushirikiano wan chi hizo tangu kuanzishwa na Rais wa awamu ya Kwanza Mwalimu Julius Nyerere mpaka sasa unauendelea.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mapokezi ya meli hizo, Kamanda wa Jeshi la Wanamaji (Navy), Rear Admiral Ameir,  Ramadhani Hassan alisema meli hizo zimekuja nchini kwa ajili ya kufanya mazoezi ya kijeshi ya pamoja kati ya vikosi vya JWTZ na  Jeshi la Ukombozi kwa lengo la kubadilishana uzoefu.


“Majeshi yetu yalishafanya mazoezi zaidi ya mara tatu katika kozi maalum lakini zoezi la mwaka huu ni kubwa zaidi kwa sababu linahusisha Vikosi vya Jeshi la Anga (Air Force), Nchi Kavu (Land Force) na Wanamaji (Navy), jana (juzi) tumeiaga  Meli Vita Matibabu, baada ya kutoa huduma ya matibabu kwa Watanzania na imeondoka leo (jana) tunazipokea hizi" alisema Rear Admiral  Hassan.


Alisema ushirikiano wa mazoezi ya pamoja JWTZ itapata faida ya kujifunza ujuzi wa kijeshi mpya kutoka kwa Jeshi la Ukombozi na pia kutaimarisha uhusiano kati yao.


Alisema hata sasa JWTZ imepeleka askari na maofisa wake nchini China kwa ajili ya masomo mbalimbali ya kijeshi na kwamba ushirikiano huo unatimiza miaka 60 tangu kuanzishwa na Mwalimu Nyerere na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan  anauendeleza.

Aidha alisema mazoezi haya yanakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 60 ya JWTZ ambayo kilele chake ni Septemba Mosi, mwaka huu.

Naye Kapteni Mwandamizi wa Jeshi la Ukombozi, Li Bo alisema wamefika nchini Tanzania kubadilishana mbinu na uzoefu wa kijeshi na JWTZ na kwamba ana imani watajenga na kuwa imara kwa pamoja.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI