Header Ads Widget

RC CHALAMILA ATOA MAAGIZO HAYA

 



 Na Matukio DaimaApp

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe AlbertAidha RC Chalamila ameagiza kuendelea kutolewa elimu na kuhamasisha watu kuacha kujenga kwenye mabonde na kuendelea kulinda kingo za mito kwa kupanda miti kandokando ya mito.


Aidha, katika kukabiliana na nyumba kusombwa na maji zilizopo kando ya mito  ameshauri ipandwe miti ya michikichi ambayo inapatikana Kigoma, hivyo katibu Tawala wa Mkoa alifanyie kazi jambo hilo


Agizo hilo amelitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua katika kikao cha bodi ya barabara na Kamati ya ushauri ya Mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa Arnatoglo Mnazi mmoja -Ilala.

 

Aidha, alipokua katika kikao hiko pamoja na mambo memgine alipokea michango na ushauri kutoka kwa wajumbe wa kikao hicho ambao ni waheshimiwa wabunge na wataalam wengine ambao walihudhuria kikao hicho.



Hata hivyo,  amewahakikishia wajumbe kulipatia suluhu tatizo la ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi ya barabara hususani ile ambayo tayari ilishatangazwa kutekelezwa, kwa hatua ya awali amemtaka Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila kuratibu timu ya watu wachache kwa ajili ya kwenda kumuona waziri mwenye dhamana. 


Sambamba na hayo, RC Chalamila ameagiza kuwapanga vizuri wafanyabiashara wadogo na maeneo ya ‘Road Reserve’ pamoja na ya wazi kuwe na ubunifu wa matumizi yenye tija na maslahi mapana kwa umma,pia wale ambao majengo yao yanaangalia barabarani washirikishwe kuweka perving na kupanda miti ya kuvutia ambayo italeta taswira nzuri ya Mkoa, hata hivyo kwenye suala la ubora na uwekaji wa viraka barabarani ameagiza kutekelezwa kwa wakati hususani zile sehemu zilizoharibiwa na mvua za El-Nino.

 

Aidha, RC Chalamila amesema kwa upande wa ulinzi na usalama mkoa uko shwari sana vitendo vichache vya kiharifu vimeendelea kudhibitiwa ambapo ametoa rai kwa kila mtu kuelimisha jamii kufuatia uzushi unaosambazwa katika mitandao ya kijami kuhusu kutekwa na ukatili dhidi ya watoto ni vizuri kutoa elimu ili kuondoa taharuki kwa jamii "suala la usalama ni jukumu letu sote tuendelee kushikamana"amesema Chalamila.

 

Aidha kikao hicho kilihudhuriwa na Kamati ya Usalama ya Mkoa, Viongozi wa chama Mkoa, TARURA, TANROAD, makatibu Tawala wa Wilaya kwa niaba ya wakuu wa Wilaya, Mameya, Katibu Tawala wa Mkoa Dkt Toba Nguvila na wataalamu wengine kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI