Header Ads Widget

TUSHIRIKIANE KATIKA KUWALEA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

 


Na Mwandishi Wetu



Jamii imeaswa kushiriki Katika kuwalea watoto yatima nawanaoishi katika mazingira magumu ili kuwapungumzia mizigo Serikali na tasisi binafsi katika malezi ya watoto hao.


Hayo yamebainishwa na sista  Deodorah Mtagona kutoka shirika la Damu takatifu ya Yesu ambaye ndiye mlezi wa watoto yatima na waishio katika mazigira magumu wa kituo cha Upendo Okat Kilichopo Njia panda Himo, Moshi Mkoani kilimanjaro.


“Ni vyema jamii ikawa na moyo wa kuwasidia watoto hawa bila kusubiri wafadhili kutoka nje ya nchi “ amesema Sista Deodorah 


Aidha ameongeza kuwa watoto wanaolelewa katika kituoni hapo chimbuko lao ni kutoka Katika kituo cha Upendo Children Home ambapo hapo hulelewa mapaka umri wa kuanza masomo ya awali ndipo wanapotawanywa katika vituo mbalimbali vya Serikali hali inayopelekea watoto hao kukosa matumaini.



“Mpaka sasa nina watoto 26, wakiume 11 na wakike 15,na watoto hawa wamepata ufadhili kutoka kwa wadau wa ndani na nje ya nchi na wapo wanaosoma shule za sekondari na shule za msingi”


Hata hivyo sista huyo ameongeza kuwa mchakato wa kuanzisha kituo hicho ulianza mwaka 2020 ambapo mfadhili kutoka Nchini Marekani Lioba Mosha ambaye ni Mhadhiri kutoka katika chuo kimoja katika Nchi hiyo alitembelea Tanzania na kukutana na masista hao ndipo wazo la kuanzisha Kituo hicho lilipoanzia.



“Mfadhili huyo alipokuja Tanzania alikuja na timu ya wanafunzi kutoka katika nchi hiyo walichukua wazo hilo na ndipo walipoanza kulifanyia kazi na mpaka sasa bado wafadhili hao wanakisimamia kituo hicho.


Sista Mtagona amebainisha kuwa licha ya watoto hao kulelewa katika maadili ndani ya kituo hicho zipo baadhi ya changamoto za kimaadili kutoka kwa watoto hao.


“Zipo tabia zigine watoto hutoka nazo mashuleni wanapokutana na watoto wengine ndio maana kituo hapo kuna sista anaye husika katika swala zima la kuwajenga kimaadili watoto hao”



Naye Mjumbe wa bodi wa kituo hicho Antony Semagi amesema Watoto waliopo katika kituo hicho ni wakitanzania hivyo Jamii yote ya Kitanzania inayo wajibu wa kuwalea watoto hao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI