WANANCHI Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Wameipigia Magoti Serikali, kuhusu Changamoto ya kukosekana kwa barabara ya Lami ya Mafinga Mgololo.
Katika nyakati tofauti ziara ya Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa,Ndg.Dickison Lutevele (Villa) Wananchi hao walimuomba aone uwezekano wa kufikisha kilio hiki cha Wananchi kwa DR.Samia Suluhu Hassan Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ndg.Villa yupo katika ziara ya kutembelea Wananchi katika majimbo ya Uchaguzi ya Mufindi Kaskazini ,Kusini na Jimbo la Mafinga ili kuzungumza na Viongozi wa CCM wa Mashina ,Matawi na Makada ili kuhamasisha kujitokeza kujiandikisha kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Daftari la kudumu la Mpiga kura mwaka huu 2024.
Ndg.Dickison Lutevele Villa pia yupo katika ziara ya kukutana na Viongozi katika mikutano ya ndani na ya hadhara kwa Wananchi wa majimbo hayo Matatu ya Mufindi Kaskazini, Mufindi Kusini na Mafinga .
Baada ya Wananchi hao katika Kata zao na nyakati tofauti walimuomba Ndg.Villa kufikisha kilio hiki kwa Dr.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ngazi zote za Wilaya,Mkoa na Taifa.
Pamoja na kuwaomba Wananchi kuwa na subira wakati changamoto zao linashughulikiwa kwa kuzingatia taratibu , kanuni na Sheria ,Wananchi hao walidai kilio chao kimekuwa hakitoi ufumbuzi
" Wananchi naomba mtambue kuwa Serikali yenu ni sikivu na inawapenda Watanzania na ndio maana mnaona miradi ya Maendeleo inaendeshwa kila Kijiji, Kata, Wilaya , Mkoa hadi Taifa" Alisema Villa.
Ni kweli ni kilio cha muda mrefu naamini Serikali imesikia na itaendelea kuchakata na kutekeleza kama inavyotekeleza na kukamilisha katika miradi Afya, Maji,Elimu na Miundo mbinu ya barabara.
Alisema amesikia kilio chao naye atawakilisha katika Uongozi wa ngazi za Juu kuanzia Wilaya ,Mkoa na Taifa kwa kuzingatia taratibu za Chama cha Mapinduzi CCM .
Awali wakiwakilisha hoja hiyo Wananchi hao akiwepo Bw.Mahamud Mgimwa (Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Mufindi Kaskazini alisema suala la barabara za lami imeendelea kuwa changamoto muda mrefu.
Aliongezza kusema Barabara ya Mafinga/Madibira/Rujewa/Igawa Mbarali inahitaji msukumo wa ziada.
Barabara hizi zimekuwa zikipigiwa kelele na Wananchi na Wabunge lakini ufumbuzi wa changamoto hiyo imebakia kaa la moto kwa kikosa utekelezaji wake.
"Hii hizi barabara tangu Mufindi ikiwa na Jimbo moja na sasa yamefikia majimbo matatu nadhani umefika wakati wa Serikali kufanya jambo kwa Mufindi.
Aidha Bw.Jackison Manga aliiomba Serikali kuona umuhimu wa kuijenga barabara hiyo kwa kiwango cha Lami hata kwa kufanyakazi hiyo hatua kwa hatua.
Bw. Manga alisema barabara husika zikijengwa kwa kiwango cha Lami itakuwa fursa kwa Wananchi na Serikali kuzalisha kwa kiwango kikubwa mazao ya Mbao, Chakula na biadhaa za Kiwanda cha karatasi cha Mufindi Paper Mills (MPM) .
Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Mufindi Ndg.Dickison Lutevele (Villa) anatarajia kukamilisha ziara hiyo Julai 22 mwaka huu kwa kufanya mkutano wa hadhara Kata ya Kinyanambo Halmashauri ya Mufindi
0 Comments