Na Ashton Balaigwa,MOROGORO
WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) unaendelea kufuatilia vibali vya ajira kwa ajili ya kuongeza wataalamu wa ununuzi wa umma katika Sekta ya ununuzi ndani ya wakala huo ili kuongeza ufanisi zaidi kwenye utoaji wa huduma hizo,
Kamishna wa Uhifadhi TFS, Profesa Dos Santos Silayo alisema hayo alipofungua mafunzo ya maandalizi ya mpango wa ununuzi pamoja na mafunzo ya ununuzi wa mwaka wa fedha 2024/2025 .
Meneja wa Ununuzi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Kamishna Msaidizi Fridolin Matembo mwenye suti,akiwa na Wahifadhi wa Wakala huo kutoka maeneo mbalimbali wakati wa maandalizi ya mpango wa ununuzi pamoja na mafunzo ya ununuzi wa mwaka wa fedha 2024/2025 yaliyofanyika mjini MorogoroMafunzo hayo yaliyowashirikisha Makamishna wa Kanda zote,Viongozi wa Ununuzi waliokasimishwa kwenye maeneo 11 kutoka wakala huo yalifanyika katika Kituo cha Uzalishaji Mbegu bora za miti mkoani Morogoro.
Profesa Silayo alisema upungufu wa wataalamu wa ununuzi wa umma katika sekta ya ununuzi ndani ya wakala , suala hilo linafanyiwa kazi kwa kuendelea kufuatilia vibali kwa ajili ya kuongeza wataalamu wa sekta hiyo.
Kuhusu kuandaliwa kwa mpango wa ununuzi , Profesa Silayo alisema kutokana na mabadiliko ya sheria ya ununuzi na kanuni zake ambazo zinaelekeza ununuzi kwa ujumla wake pamoja na sheria ya fedha na kanuni zake ambazo ziligusa jinsi ya utendaji mali , imeonekana ni vema kuandaliwa wa mafunzi ili kujenga ulewa ili mpango wa ununuzi uandaliwe kwa kuzingatia maboreshi ya sheria yaliyopo .
Profesa Silayo alisema kila mwaka bajeti ya ununuzi na ugavi ya Wakala huongezwa kadiri inavyofaa mfano kwa mwaka huu wa fedha bajeti imeongezwa kutoka milioni 300 mpaka milioni 600.
“ Kwakuwa ununuzi unachukua zaidi ya asilimia 70 ya bajeti ya Serikali ni vyema mpango huu wa ununuzi ukaandaliwa kwa ufanisi na weledi wa kutosha ili uweza kuingizwa katika vikao kwa ajili ya kupitishwa “Alisema Profesa Silayo
Profesa Silayo aliwataka watalaam wa manunuzi utii wa sheria na kanuni uzingatiwe katika ngazi zote za kitaasisi.
Naye Meneja wa ununuzi Kamishna Msaidizi wa TFS Fridolin Matembo,alisema mafunzo hayo ni kuongeza ufanisi na ulewa mpana kuhusu mifumo mipya ya serikali katika masuala ya manunuzi itakayosaidia kuokoa fedha za serikali kwenye matumizi yasiyo ya lazima.
Alisema kwa mujibu wa taratibu za serikali kwenye masuala ya ununuzi tayari wameanzisha kitengo cha ununuzi ambacho kimesaidia kutumia mfumo wa Kitroniki kadri ya serikali ilivyoelekeza na kufikia asilimia 100 mfumo mpya wa manunuzi ya Umma(NeST) ,Mfumo wa ulipaji Serikalini (MUSE) ,mfumo Jumuishi wa Kietroniki katika utoaji wa huduma za wakala wa huduma wa ununuzi Serikalini( GIMIS),Wakala wa huduma ya ununuzi Serikali (GPSA), mifumo ya ndani ya TFS imesaidia kwenye usimamizi.
Alisema kupitia mifumo hiyo mipya imesaidia kwenye usimamizi katika maeneo mbalimbali ya Wakala huo kwani isingekuwepo mifumo hiyo wangelazimika kupeleka watumishi na kulipa gharama kubwa .
“ Hii Mifumo mipya imepunguza gharama za fedha za serikali na kufanikiwa kufika maeneo yote na kufanikisha masuala ya ununuzi wa Umma kwa kutumia eletroniki “ alisema Matembo.
Kamishna huyo Msaidizi wa TFS Matembo,alisema baada ya watalaam kupata ulewa wa matumizi ya mifumo hiyo,wanakwenda kuandaa mpango wa mwaka wa ununuzi kwaajili ya kuhakikisha manunuzi ya mwaka wa fedha 2024/25 yanatekelezwa ipasavyo kwa kuzingatia sheria,kanuni na taratibu .
Katika hatua nyingine aliishukur Serikali kwa kufanikiwa ujenzi wa Ofisi za Makamishna ngazi za wilaya katika kila mkoa kuna zaidi ya ofisi moja ,kujenga nyumba za dharura za kuishi askari wa kudhibiti ujangili na kuongeza ulinzi wa maliasili zilizopo kwenye hifadhi mbalimbali.
Mwisho.
0 Comments