Header Ads Widget

TAMASHA LA USAMBARA TOURISM FESTIVAL LASOGEZWA MBELE


Na Ashrack Miraji (Matukio Daima App)Lushoto Tanga 

Mkuu wa wilaya ya Lushoto,Mkoani Tanga,Jafar kubecha amewaomba radhi wananchi na wageni wote waliotarajia kuja kwenye tamasha la  kitalii la "Usambara Tourism Festival" lenye lengo la kukuza uchumi hasa kwenye sekta ya utalii wilayani hapo.


Kubecha amesema tamasha hilo ambalo lilipagwa kufanyika  Julai  25-27 mwaka huu kuwa  limesogezwa mbele kutoka na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wao,hivyo tamasha hilo litafanyika Septemba 6 - 7  mwaka huu.


"nitumie fulsa hii kuwapa pole wananchi na wageni wetu ambao tuliwatarajia kushiriki kwenye tamasha letu kuja kujionea vivutio mbalimbali vya kitalii na majengo makubwa ambayo yalijegwa na mjerumani hususani jengo la Mkuu wa Wilaya ya Lushoto" alisema Kubecha.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI