Header Ads Widget

RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN ATOA MASHUKA KWA AJILI YA KITUO CHA AFYA PASUA.

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI. 


MBUNGE wa viti maalum kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Zuena Bushiri amekabidhi mashuka yaliyotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kituo cha Afya cha Pasua kilichopo manispaa ya Moshi lengo likiwa ni kuendelea kuboresha huduma za Afya kwa Wananchi. 



Zuena alikabidhi mashuka hayo leo ambapo alisema kuwa, Rais Dkt. Samia katika kuonyesha anawajali Wananchi wake ametoa mashuka hayo ambapo Mbunge huyo aliyakabidhi kwa wodi ya mama na mtoto. 



Alisema kuwa, serikali ya awamu ya sita imeweza kuboresha miundombinu ya Afya kwa kuhakikisha vifaa tiba na dawa zinapatikana katika ngazi zote kuanzia zahanati, vituo vya Afya hospitali za wilaya, mikoa na hospitali za rufaa. 


" Nimesikia katika rasala yenu itabidi ya wagonjwa wanaohudumiwa katika kituo hiki cha Afya ni kubwa kwani inahudumia kata zaidi ya saba za manispaa ya Moshi lakini pia wagonjwa wengine wanatoka nje ya manispaa na mkoa hasa wakinamama wajawazito wanaokuja kujifungua hii ni kutokana na huduma nzuri na bora mnazozitoa katika kituo hiki niwapongezeni sana" Alisema Mbunge huyo. 



Awali akisoma risala ya kituo hicho kwa Mbunge, Tujanaeli walisema kuwa idadi ya Wakinamama wanaojifungulia katika kituo hicho ni wastani wa 35 kwa mwezi huku idadi ya wanaofanyiwa upasuaji ikiwa ni 60 kwa mwezi huku wanakimama wanaolazwa kusubiria kujifungua ikiwa ni 300 kwa mwezi. 



Alisema kuwa, kwa sasa kituo hicho kinakabiliwa na uchakavu wa wodi ya wanawake na wodi ya watoto, ukamilishaji wa uzio kuzunguka eneo la kituo kwa ajili ya usalama  pamoja na vifaa visaidizi kwa watoto wanapozaliwa wakiwa na changamoto. 


Mwisho. ..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI