Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan aguswa
na Mwanafunzi wa Darasa la Tatu Shule ya Msingi Tunduma, Ebenezer Mwakasyele (8) ambaye ni mlemavu na kuagiza Ofisi yake pamoja na Wizara ya Afya kuhakikisha Mtoto huyo anatengenezewa mguu wa bandia mara moja.
Mwanafunzi huyo alikuwa ni miongoni mwa watu waliojitokeza kumlaki na kumsikiliza Rais wakati akiwahutubia wananchi wa Tunduma, Mkoani Songwe, leo Julai 18, 2024.
Rais Dkt. Samia alisimama katika mji huo wa Tunduma kwa lengo la kuwasalimia wananchi akiwa njiani kuelekea Dodoma Mara baada ya Kumaliza Ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Katavi na Rukwa.
0 Comments