Header Ads Widget

NDERIANANGA AZINDUA MPANGO NA MKAKATI WA KUPUNGUZA VIATARISHI VYA MAAFA NCHINI

Naibu waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Ndariananga amefanya uzinduzi wa nyaraka za usimamizi  wa maafa wilaya ya Kibiti kwa lengo la kusimamia na kuratibu shughuli za kuzuia na kukabiliana na majanga nchini.


Akizungumza kabla ya kuzindua Nyaraka za Usimamizi wa Maafa Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani na kuhusisha Viongozi mbalimbali wa wilaya ya Kibiti na mkoa wa Pwani amesema moja ya majukumu ya Idara ya Menejimenti ya Maafa kupitia Sheria ya Usimamizi wa Maafa namba 6 ya Mwaka 2022 ni kutayarisha, kuhuisha na kuratibu utekelezaji wa sera, mipango, sheria, kanuni, mikakati na taratibu za utendaji kwenye shughuli zote zinazohusiana na usimamizi wa maafa Tanzania Bara.


Ndariananga amesema mpango wa serikali ni kukabiliana na maafa nchi mzima , lakini imeanza na wilaya kibiti kwa kushirikiana na UNDP ili kuweza kujikinga  na maafa, huku akikaribisha wadau mbalimbali katika kushirikiana na serikali ili kuweza kufikia malengo.


Ndariananga amesema kuwa nyaraka ambazo zimezinduliwa ziende zikatumike katika kutendea kazi  kikamilifu huku akisisitiza kuwa kazi imeanza mara baada ya uzinduzi huo.


Aidha Mhe. Ummy amesema kazi ya uandaaji wa mpango wa kujiandaa na kukabiliana na maafa na Mkakati wa Kupunguza Viatarishi vya Maafa kwa Wilaya ya Kibiti ni muendelezo wa utekelezaji wa jukumu hilo la msingi la Ofisi ya Waziri Mkuu ambalo limelenga kuimarisha usimamizi na uratibu wa Maafa katika ngazi za Mikoa na Wilaya.


"Kama mnavyofahamu katika kipindi cha mwezi Januari hadi Mei, 2024 mvua kubwa zilizonyesha katika maeneo mbalimbali Nchini na kusababisha Maafa ya Mafuriko katika maeneo mengi ikiwemo Mkoa wa Pwani Mafuriko haya yalisababisha madhara mbalimbali ikiwemo vifo, majeruhi, uharibifu wa mali, miundombinu na mazingira," alisema Ummy


Aliongezea kuwa kufuatia hali hiyo Serikali kwa kushirikiana na wadau ilichukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuratibu upatikanaji wa misaada ya kibinadamu kwa waathirika, kuimarisha huduma za Afya, kutoa huduma ya Afya ya akili na msaada wa kisaikolojia na kijamii, kuratibu na kutekeleza operesheni ya utafutaji na uokoaji, kutafuta, kukusanya na kugawa misaada ya kibinadamu na kurejesha miundombinu iliyoathirika.


Katika hatua nyingine Ummy ametoa wito kwa wahusika kuhakikisha nyaraha hizo zilizoandaliwa ziwe ni chachu ya kuongeza ushirikishwaji wa jamii na wadau Pia, kujenga uelewa wa jamii kuhusu masuala ya usimamizi wa maafa, kuimarisha mfumo wa utoaji tahadhari ya awali, kujenga uwezo wa kuzuia, kupunguza madhara na kujiandaa na maafa na kujenga uwezo wa kukabiliana na maafa.


Sambamba na hilo Naibu Waziri, amemtaka mkuu wa wilaya ya kibiti Kanali Joseph Kolombo, kuweka mikakati madhubuti katika wilaya na kuendeleza Yale waliyojifunza katika kujikinga na maafa huku akitoa wito kwa Idara, vitengo na taasisi zote katika utekelezaji wa kisekta.


Kwa upande wake mkurugenzi   Idara ya menejimenti ya maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu  Brig.  General  Hosea  Ndagala, amesema kuwa wanaendelea kuimarisha utekelezaji katika ngazi ya wilaya kupitia mafunzo yanayotolewa.


Nae mtaalam wa miradi UNDP Abbas Kitogo amesema kuwa nyaraka hizo ni chachu kwa jamii  katika kukabiriana na majanga mbalimbali, huku akisisitiza kuwa UNDP itaendelea kushirikiana na serikali katika kupambana na majanga.


UNDP  imepokea shilingi Billion 23 kwa ajili ya  kukabiliana na  maafa kwa kushirikiana na mamlaka ya Hali ya Hewa TMA.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI