Header Ads Widget

NDEJEMBI MA_RC WAAGIZWA KUANZISHA OPERESHENI KUKAMATA WAGANGA WAPIGA RAMLI CHONGANISHI


Na Mariam Kagenda  - Kagera

Wakuu wa Mikoa nchini wameagizwa kufanya operesheni ya kukamata waganga wa tiba asili na tiba mbadala wasio na leseni ambao wanajihusisha na ramli chonganishi zinazochangia vitendo vya kikatili dhidi ya Watu wenye Ualbino.

Maelekezo hayo yametolewa na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Deogratius Ndejembi leo Julai 9, 2024 Mkoani Kagera wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya kupinga ukatili dhidi ya watu Wenye Ualbino iliyozinduliwa katika kata ya Kamachumu mkoani Kagera  ambayo imeambatana  na kauli mbiu  isemayo “Mimi nipo  ninapinga ukatili dhidi ya watu Wenye Ualbino”

Vile vile, Mhe. Ndejembi amewataka Wakuu hao wa Mikoa kuhakikisha wanafanya kampeni ya kupinga ukatili dhidi ya watu wenye Ualbino katika Halmashauri zote na kuhakikisha kamati za watu wenye ulemavu zinaimarishwa katika maeneo yao kwani ni takwa la kisheria kupitia sheria namba 19 ya mwaka 2010 ya watu Wenye Ulemavu. 

 Mhe. Ndejembi  Pia ametoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Kagera  kuwa Mabalozi wa ulinzi wa Mtu Mwenye Ualbino kwa kutoa elimu, kupinga ukatili na kutoa taarifa kwa viongzo pale wanaposikia ama kuona viashiria vya ukatili dhidi ya watu hao.

Uzinduzi huo umefanyika ikiwa ni siku chache tangu mtoto Asimwe Novath mwenye umri wa miaka 2 na nusu mwenye  Ualbino  kuuwawa kisha mwili wake kutupwa kwenye Karavati 

Awali akizungumza Mkuu wa Mkoa wa  wa Kagera Mhe. Fatma Mwassa amesema ataendelea kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama kuhakikisha vitendo vya ukatili dhidi ya  watu wenye Ualbino vinakomeshwa Mkoani humo.

Makamu Mwenyekiti wa chama cha watu wenye Ualbino Tanzania Alfred Kapole  akizungumza na wananchi wa mkoa wa Kagera wakati wa uzinduzi wa Kampeini ya Kitaifa ya kupinga ukatili dhidi ya watu wenye Ualbino


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI