Na Shemsa Mussa, Kagera
Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajati Fatuma Mwasa amekataa ombi la halmashauri ya manispaa ya Bukoba la kujenga fremu za maduka kwenye eneo la uwanja wa mashujaa maarufu kama (mayunga) akidai kufanya hivyo ni kuwavunjia heshima mashujaa waliopigana vita ya Kagera.
Amesema hayo wakati akiwahutubia wananchi katika maadhimisho ya siku ya mashujaa iliyofanyika kimkoa katika uwanja huo ambapo amesema kuwa alipokea maombi ya halmashauri hiyo lakini ameona si busara kuwavunjia heshima mashujaa na katika uongozi wake hatoruhusu jambo hilo.
Amesema kuwa katika mwaka huu wa fedha serikali ya mkoa ina mpango wa kuboresha uwanja huo kwa kujenga uzio imara na kuweka miundombunu ya kisasa kama vyoo, jukwaa na kuboresha mazingira kwa kuotesha nyasi na kupanda bustani ya maua huku akitumia nafasi hiyo kuiangiza manispaa kutafuta maeneo mengine ya kujenga flemu hizo.
"Tusikubari mipango ambayo Haina baraka za Mungu eneo hili katika kipindi Mimi nipo akija mwingine akavunja sawa lakini kipindi nipo nitajenga uzio,tutaboresha mnara Wetu, tutaboresha jukwaa,tutajenga vyoo vya kisasa na bustani nzuri ili kuendelea kuwaenzi Mashujaa Wetu kanunueni Viwanja sehemu nyingine mjenge frem ila sio hapa ,amesema Mhe Fatuma"
Kwa upande wao baadhi ya mashujaa waliopigana vita ya Kagera akiwemo Dauda Kakuba na Gabriel Elias wamempongeza mkuu huyo wa mkoa kwa kuendelea kulinda eneo hilo huku wakiwashauri vijana wa jeshi kuwa wazalendo kwa kulilinda taifa la Tanzania.
Pia Mashujaa hao wamechukua nafasi hiyo kuwaomba Wastaafu na wazee wote kuwa walezi kwa vijana kufanya kazi kwa bidii na kujitoa na kujituma ili kuepuka kuombaoba na kuwa tegemezi kuepuka madhara ya kutawaliwa.
Ikumbukwe kuwa Maadhimisho ya mashujaa huadhimishwa Kila siku ya Tarehe 25 July Kila Mwaka .
1 Comments
Kazi nzuri sana
ReplyDelete