Header Ads Widget

MBUNGE NJEZA AHIMIZA UCHAGUZI, CCM KUSHINDA 2024 MBEYA VIJIJINI.

NA JOSEA SINKALA, MBEYA.

Mbunge wa Jimbo la Mbeya vijijini Mhe. Oran Njeza, anaendelea na ziara ya kukagua miradi, kuzungumza na wananchi wake na kuwahimiza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili kuchagua viongozi bora kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, vitongoji na vijiji baadaye mwaka huu.


Mbunge Njeza ameendelea na ziara hiyo katika vijiji vya Mapita na Inuka kata ya Izyira ambako kote ameendelea kuhimiza wananchi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye daftari la mkazi la wapiga kura ili kutimiza haki yao kuchagua viongozi wanaowataka.

Akizungumza na wananchi vijiji vya Inuka na Mapita kwa wakati tofauti, Mbunge wa Mbeya vijijini amesema kwa namna Serikali ilivyotekeleza miradi mbalimbali, inaipa nafasi kubwa CCM kushinda uchaguzi ujao wa Serikali za mitaa, vitongoji na vijiji.


Mbunge Njeza amesema Chama Cha Mapinduzi kimeendelea kuisimamia Serikali kufanya kazi kwa bidii kwa maslahi mapana ya wananchi hivyo kuwaomba wananchi kuichagua CCM kwenye uchaguzi huo.

Amesema katika kata ya Izyira pekee fedha zaidi ya shilingi billion tatu ambapo miradi lukuki inaendelea kutekelezwa.


Amesema wananchi wanazo sababu mbalimbali kuichagua CCM kwenye uchaguzi wa mwaka huu ikiwa ni maandalizi na matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwakani akitolea mfano usambazaji wa nishati ya umeme ambao sasa umefika katika vijiji vyote sasa unaelezwa kuanza kwenda vitongojini, uboreshaji miundombinu ya barabara na ujenzi wa madaraja, usambazaji wa pembejeo za kilimo, uboreshaji sekta ya elimu na mengineyo kadhaa.

Mbunge huyo amewaasa wananchi kuchagua viongozi bora kwenye uchaguzi huo na kusisitiza kuwa anaamini viongozi bora watatoka Chama Cha Mapinduzi (CCM).


"Ndugu zangu na mimi nimekuja kubwa zaidi kuwahimiza mwaka huu tuna uchaguzi, tuhakikishe tunahamasika na tukahakikishe taarifa zetu kwenye daftari la wapiga kura. Tukachague viongozi wazuri, wewe usiangalie sura ya mtu tunachohitaji ni maendeleo lakini imani yangu viongozi wazuri watatoka CCM", amesema Mbunge Oran Njeza wa Mbeya vijijini.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Izyira Mhe. Abeli Mwazembe, amemshukuru Mbunge wa Mbeya vijijini kwa kuendelea kuiomba Serikali kutoa fedha ili kutekeleza miradi mbalimbali kwa manufaa ya wananchi akiahidi kuendelea kuhimiza wananchi kushiriki uchaguzi wa mwaka huu na kuhimiza kuichagua CCM.


Ikumbukwe kuwa Tanzania inatarajia kuingia kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, vitongoji na vijiji baadaye mwaka huu (2024) ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaendelea kuhimiza wananchi kushiriki uchaguzi huo kwa kuchagua viongozi bora watakaosimamishwa na CCM badala ya vyama vya upinzani.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI