Header Ads Widget

MAWAKALA WA MIAMALA YA FEDHA MKOANI NJOMBE WALALAMIKIA USHIRIKIANO DUNI WA JESHI LA POLISI

 






Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimAPP NJOMBE

Serikali mkoani Njombe imesema hakuna biashara itakayofungwa saa 12 jioni kwa kuhofia wezi na majambazi kwani Jeshi la polisi liko imara katika kukabiliana na uhalifu wa aina yoyote.


Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wafanyabiashara hususani mawakala wa miamala ya fedha na kwamba biashara zitafanyika kwa saa 24 na ulinzi umeimarishwa.


Aidha Mtaka amewataka wafanyabiashara hao kubadilika na kufanyakazi Kidigitali kwani dunia ya sasa ipo kiganjani hivyo wanapaswa kufunga camera za Ulinzi[CCTV CAMERA] Ili kupunguza changamoto za usalama wa Raia na mali zao.


Baadhi ya wafanyabiashara mkoani Njombe akiwemo Bahati Govela,Elly Ngole,Gervas Mangula na Anna Mayemba wameomba jeshi la polisi kuchukua hatua haraka kwani kuna baadhi ya matukio ambayo yamekuwa yakijirudia lakini wahalifu hawakamatwi kwa wakati jambo ambalo linasababisha madhara makubwa.


Wengine wamelitupia lawama jeshi la Polisi kwa kushindwa kuwabaina wahalifu licha ya kuwasilisha baadhi ya vielelezo muhimu huku matukio yakiendelea kujirudia. 


Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga akitolea ufafanuzi wa malalamiko ya wahanga hao amekiri kupokea malalamiko hayo na kwamba atakwenda kuyapitia majalada yote na kuchukua hatua.


Hatua hiyo inakuja kufuatia matukio ya mauaji na uporaji wa fedha kwa wafanyabiashara mbalimbali wakiwemo wa miamala ya fedha ikiwa julai 20 mwaka huu mmoja wa wakala mkubwa Godfrey Ndambo aliuawa na kuporwa shilingi milioni 47 wakati anataka kuingia nyumbani kwake huko Uzunguni Ramadhani.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI