Thobias Andengeye Mkuu wa mkoa Kigoma
Chanzo cha maji cha Amani Beach Manispaa ya Kigoma Ujiji kinachotumika kwa ajili ya kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa manispaa ya Kigoma Ujiji na vitongoji vyake
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kigoma (KUWASA) imesema kuwa imeweza kutekeleza kwa vitendo azma ya serikali ya kumtua mama ndoo kwa kuweza kufikisha huduma ya maji karibu na makazi ya wananchi katika halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji na vitongoji vyake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo, Poas Kilangi alisema hayo akizungumza na waandishi wa Habari waliofanya ziara kutembelea mradi mkubwa wa maji ikiwemo chanzo cha maji cha Amani Beach.
Kilangi alisema kuwa mamlaka hiyo imeweza kukamilisha mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya shilingi Bilioni 42 ambao umewezesha uzalishaji maji kufikia lita milioni 42 kwa siku ambapo kwa sasa upatikanaji maji safi na salama kwa manispaa ya Kigoma Ujiji imefikia asilimia 92.
Alisema kuwa baada ya kukamilika kwa mradi huo kwa sasa wanapambana na uboreshaji wa miundo mbinu ya maji Kwenda kwa wananchi kutokana na mkiundo mbinu ya awali kuchakaa ambapo mpango huo unatarajiwa kuifanya mamalaka hiyo
Akizungumzia hali ya upatikanaji wa maji katika manispaa ya Kigoma Ujiji Mkuu wa mkoa Kigoma,Thobias Andengenye alisema kuwa kwa sasa hali ya upatikanaji wa maji Kigoma Ujiji ni nzuri na kuipongeza KUWASA kwa kazi nzuri ya kupeleka maji kwa wananchi na kuondoa changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji safi na salama uliokuwepo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa wa Katonga Manispaa ya Kigoma Ujiji, Damas Shatiel alisema kuwa kwa sasa hali ya upatikanaji maji ni nzuri na wanaishukuru KUWASA kutekelezaji mradi mkubwa wa maji ambao umewezesha maji safi na salama kupatikana bila shida na kuondoa changamoto ya watu kutembelea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.
Mwisho.
0 Comments