Header Ads Widget

BYABATO KUTOA KOMPYUTA MPAKATO .

 



Na Mariam Kagenda ,Kagera

 Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Wakili Stephen Lujwahuka Byabato anatarajia kutoa Kompyuta mpakato (LAPTOP) zipatazo 109 ili kuendelea kukuza kiwango cha Taaluma katika halmashauri ya Manispaa ya Bukoba 


 Katika jitihada za Kuunga Mkono Juhudi za Serikali katika Sekta ya Elimu kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba Mbunge huyo  atatoa kompyuta Mpakato (LAPTOP) kwa  Watendaji  wa kata, Waratibu kata, Wakuu wa Shule  za Sekondari na   Binafsi pamoja na Walimu Wakuu wa Shule za Msingi za Serikali na Binafsi  kulingana na Idadi yao Ili zisaidie katika jitihada za kuinua Kiwango Cha Elimu na Ufaulu kwa wanafunzi wa  halmashauri ya Manispaa hiyo.



Hayo yameelezwa na Katibu wa Mbunge  Ndg. Pasaka Bakari wakati akichangia katika Majadiliano ya Kikao cha Wadau wa Elimu mkoani Kagera chini ya Mwenyekiti wake Hajat Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa Kagera, chenye lengo la Kutathimini kiwago cha Elimu  na Kuweka mikakati ya kuongeza Kiwango Cha ufaulu.


Ndg. Pasaka aliyemuwakilisha Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Stephen   Byabato Kutokana na udhuru ya Kikazi  amesema kuwa   Mbunge huyo  Byabato anatarajia  kukabidhi Laptop 109 kwa Wahusika hao kwa kila Kata pamoja na Shule hizo, Ili zisaidie katika Masuala ya kitaaluma.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI