Header Ads Widget

KUNENGE ASEMA MNARA WA MASHUJAA NI KUENZI MASHUJAA WALIOPIGANIA NCHI.

 


KUJENGWA kwa mnara mrefu wa Kumbukumbu ya Mashujaa Mkoani Dodoma ni kuthamini mashujaa waliolipigania Taifa letu.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge wakati wa kuadhimisha Kumbukumbu ya Mashujaa kimkoa iliyofanyika mjini Kibaha.



Kunenge amesema kuwa mnara huo unaonyesha jinsi gani Taifa linavyothamini mchango wa mashujaa hao wa Tanzania.


"Wakati tukiendelea kuwakumbuka na kuwaombea mashujaa wetu tumwombee na Rais kwa kuendelea kuwaenzi kupitia mnara huo,"amesema Kunenge.


Kwa upande wake Mchungaji Julius Shemkai amesema kuwa mashujaa hao lazima wapongezwe kwani walipambania nchi na wale wote wenye nia mbaya wasindwe ili nchi iendelee kuwa na amani.


Sheikh Said Chega amesema kuwa wanamwombea Rais ili aweze kuongoza kwa amani na kutekeleza vyema majukumu yake na nchi iendelee kubaki salama.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI