WAKILI maarufu wa kujitegemea nchini Boniface Mwabukusi amesema wakati anapata taarifa ya kuenguliwa kugombea nafasi ya Rais wa TLS (Chama cha Mawakili Tanganyika) na kamati ya rufani ya chama hicho hakuamini kama Mawakili wenzake wanaweza kufanya dhulma ya aina hiyo dhidi yake kwa kuwa aliona wazi maamuzi hayo hayakuwa ya haki na hayakufuata misingi ya kisheria ndio maana hata wahusika hawakumpatia nafasi ya kujitetea
Wakili Mwabukusi amezungumza hayo leo, Ijumaa Julai 26.2024 mbele ya wanahabari muda mfupi baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam kutengua maamuzi ya kamati hiyo na kumrejesha Wakili Mwabukusi kugombea nafasi ya Rais wa TLS katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao
Kwa upande wake Wakili Jebra Kambole aliyekuwa anamtetea Wakili Mwabukusi katika kesi hiyo sambamba na Mawakili wenzake 18 ametoa wito kwa mamlaka mbalimbali zinazotoa maamuzi nchini ni lazima zizingatie misingi ya kisheria katika maamuzi yao badala ya kutumia nafasi walizonazo kuumiza wengine,
Chanzo:Jambo
0 Comments