Na Fadhili Abdallah, Kigoma
CHAMA cha ACT Wazalendo kimeanza mchakato wa kusajili wanachama milioni 10 ili kuwageuza kuwa wapiga kuwezesha chama hicho kushinda uchaguzi mkuu mwaka 2025 na kushika dola.
Kiongozi wa Chama Mstaafu, Zitto Kabwe akisema hayo akihutubia mkutako wa hadhara kwenye eneo la Rasini Kibirizi Manispaa ya Kigoma Ujiji akianza ziara ya mikoa saba ya kanda ya Magharibi ambapo atatembelea na kufanya mikutano katika majimbo 36.
Kabwe alisema katika kampeni hiyo ya mikoa 22 kutembelea majimbo 244 watatembea na kufanya mikutano kwenye majimbo hayo wakiwa wamegawanyika timu tatu za viongozi wa chama hicho na kwa upande wake ameazna mikutano mkoa Kigoma ambayo inatamwezesha kufanya mikutano katika majimbo nane ya mkoa Kigoma.
Alisema kuwa wameanza kusajiili wanachama kupitia mpango wa ACT kiganjani na Kutokana na hilo kiongozi huyo amehamasisha watanzania kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwani ndiyo mahali pekee ambapo wanaweza kupata ushindi kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu.
“Tumeanza ziara ya viongozi wakuu wa Chama cha ACT kutembelea mikoa 22 na kufanya mikutano kwenye majimbo 224 mikutano ambayo itatuwezesha kusajili wanachama milioni ambao hao watakuwa wapiga kura wetu kwenye uchaguzi watakaiwezesha chama kushinda uchaguzi na kushika dola,”Alisema Zitto Kabwe.
Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo mkoa Kigoma,Kiza Mayeye aliwaomba wananchi wa mkoa Kigoma kujiandikisha kuwa wananchama wa Chama hicho kupitia mfumo wa ACT Kiganjani ili kukifanya cha hicho kuwa na wanachama wengi ambao watakuwa wapiga kura na kuwezesha mpango wa kushika dola na kuondoa CCM madarakani.
Mayeye alisema kuwa lazima wananchi wastuke na madhira makubwa yanayofanywa hasa matunizi ya nguvu kupita kiasi ya polisi na vitendo vya kupotea kwa wakati kwenye mikono ya polisi huku viongozi wa jeshi hilo wakikanusha kuhusika na udhalimu humo.
0 Comments