Header Ads Widget

WENYE UALBINO NENDENI TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD KUNA FURSA ZA BURE KWAAJILI YENU - DKT. MAGUHA

 


Wito umetolewa kwa watu wenye ualbino kufika katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kupata huduma za afya iliwaweze kunufaika na fursa mbali mbali zinazotolewa na serikali ikiwemo vipimo na mafuta kinga bure kwaajili yao.


Hayo yamesemwa na Daktari wa Kinga ya Magonjwa ya saratani wa taasisi ya Ocean Road Dkt Maguha Stefano wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha mkoani Pwani kwenye kilele cha maadhimisho ya kitaifa ya kuongeza uelewa juu ya ualbino duniani katika viwanja vya Mailmoja kibaha mkoani Pwani.


Alisema wanaofika hoispitalini hapo ni wachache hivyo amewataka watu wenye ualbino kujitokeza kwa wingi hospitalini hapo ili waweze kuhudumiwa huduma mbali mbali kwa usalama wa maisha yao.


Amesema taasisi hiyo imekuwa ikitoa elimu katika maonyesho ya maadhimisho hayo ambapo wamewapa elimu ya kujiepusha na kukaa muda mrefu kwenye jua ili wasipatwe na saratani ya ngozi ambayo imekuwa ikiwashambulia zaidi.


"Lakini pia tumeweza tunawashauri kuwa na tabia ya kupima afya yao ya ngozi mara kwa mara kwa kufika taasisi ya saratani ocean Road ambao huwa tuna kliniki ya ngozi kwa watu wenye ualbino kila alhamisi hivyo wawe wanakuja kila ambavyo wanashauriwa na Daktari ambapo angalau waje kila baada ya miezi sita kucheki afya za ngozi zao" alisema Daktari Maguha.


Aidha alisema taasisi hiyo hutoa huduma ya uchunguzi wa saratani ya ngozi kwa wenye ualbino hivyo amewataka wenye viashilia vya salatani ya ngozi wanaowahi taasisi hiyo hutoa tiba.


Kwa wanaowahi kuja kupata matibabu tunatoa tiba ya kjuzuia chembe chembe hai kugawanyika na kuwa saratani ya ngozi kwa wenye ualbino na kupatiwa fulsa ya kupewa mafuta kinga bure lakini ni wachache hujitokeza kuja kupata huduma 



Akizungumzia aina zingine za huduma za upimaji wa saratani kwa watu wenye ualbino Daktari Maguha alisema taasisi hiyo hutoa huduma ya kupima saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya matiti na saratani ya tezi dume ambapo katika maadhimisho hayo zaidi ya watu 300 wamepimwa saratani za aina mbalimbali.


"Na kuanza kuwapa matibabu wale ambao wamegundulika wapo katika hatua za awali za saratani hususani saratani ya mlango wa kizazi kinamama zaidi ya 100 wamepimwa ambapo kati yao wawili wameonekana wana dalili za awali za salatani ya mlango wa kizazi, saratani ya matiti tumepima akinamama zaidi ya 70 ambao hatujaona kitu chochote ambacho kina ashiria saratani"



"Na kwa upande wa kinababa, zaidi ya kinababa 60 wamefanyiwa uchunguzi wa saratani ya tezi dume na baba mmoja tu ameonekana ana viashilia vya saratani ambaye amepewa rufaa ya kwenda Ocean Road kwenda kufanyiwa vipimo zaidi" alisema Daktari Maguha.    


"Na pia wawe wanapima mafuta kinga na kuvaa nguo zinazokinga eneo kubwa la mwili yaani kama ni shati wavae mashati yenye mikono mirefu, suruali, kuvaa kofia zenye kingo pana ili kuweza kuwakinga na mionzi ya jua isipige maeneo ya kichwani hususani masikio na shingoni" alisema Daktari Maguha.


Naye Mkurugenzi wa Idara ya Kinga wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Daktari Chrispin Kahesa amesema taasisi hiyo imejiwekea mkakati maalumu wa kufikia jamii kwa kutoa elimu mashuleni, tiba za awali kwa kushirikiana na taasisi ya watu wenye ualbino nchini TAS ambao wameandaa mtaala maalumu ya utoaji wa elimu.



Alisema wanazunguka katika shule mbalimbali za msingi na sekondari nchini kutoa elimu walitoa elimu ya taadhari ya kupata saratani ya ngozi na kuwapa nasaha ya kuona jinsi gani watapunguza kuweza kuongezeka kwa saratani ya ngozi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI