Header Ads Widget

AJALI:RAS KILIMANJARO NA DEREVA WAKE WAFARIKI KWA AJALI




RAS KILIMANJARO AFARIKI DUNIA KWA AJALI. 

NA WILLIUM PAUL, HAI. 



KATIBU Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, Tixon Nzunda na dereva wake wamefariki dunia katika ajali ambayo imetokea eneo la Njia panda ya KIA, Wilaya ya Hai,  akiwa kwenye ziara Mkoani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo na kwamba ajali hiyo imetokea  muda wa saa 8 kuelekea saa 9 mchana leo, Juni 18, 2024.


"Ni kweli wakati anatoka KIA amepata ajali mbaya sana, ndio na mimi nakwenda eneo la ajali,"amesema RC Babu 



Muda mfupi kabla ya ajali hiyo, alikuwa na kikao na wadau wa maendeleo kutoka nchini Namibia kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

Katika ajali hiyo inadaiwa kuwa, dereva wake naye kafariki duniani.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI