Na Moses Ng'wat,Tunduma.
HALMASHAURI ya Mji Tunduma, Mkoani Songwe, imefanikiwa kununua gari la Zimamoto kwa gharama ya zaidi ya Sh 396.6 milioni kwa fedha za mapato ya ndani.
Hatua ya ununuzi wa gari hilo ni utekelezaji wa makubaliano ya vikao vya Halmashauri hiyo kwa lengo la kukabiliana na majanga ya moto katika Mji wa Tunduma wenye pilika nyingi za shughuli za biashara na malori mengi ya mizigo ambayo hupita kwenda na kuingia katika mji huo kutoka nchi za kusini mwa Afrika na Kongo.
Lakini pia Halmashauri hiyo itaondokana na adha ya kutegemea gari ya zimamoto na uokoaji kutoka nchi jirani ya Zambia.
Mkurugezi mtendaji wa Halmashauri hiyo amesema Mariam Chaulembo amesema katika bajeti ya mwaka 2023-2024 kupitia mapato ya ndani waliweka kipaumbele kwa ajili ya kununua magari mawili likiwepo la zimamoto na uokoaji kutokana mji huo kuwa na historia ya kukumbwa na matukio kama ilivyotokea katika miaka ya 2011 na 2020 ambapo milipuko ya moto iliteketeza maduka na vibanda katika masoko ya mji huo
"Gari hili linauwezo wa kumwaga maji lita elfu tano(5,000) kwa dakika tano hivyo itapunguza majanga ya moto Kwa wakazi wa Tunduma na maeneo jirani," amesema Chaurembo.
Aidha, Chaulembo amesema wamefanikiwa kununua gari la mapato Toyota Hilux kwa kutumia mapato ya ndani kwa gharama ya Sh127.3 ambayo itasaidia kupitia vyanzo vya mapato ili kuongeza wigo wa fedha.
Kwa upande wake kaiku Kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Songwe Eliutelly Mremi amesema kwa mwaka 2022_2023 matukio 17 ya moto a uokoai yalitokea Tunduma hivyo gari hilitakuwa msaada kwa wananchi.
Akizindua gari hilo Mkuu wa Mkoa huo, Daniel Chongolo, amesema ununuzi wa gari hilo utasaidia kuondoa changamoto ya majanga ya moto ambayo kwa miaka ya nyuma wafanyabiashara walipoteza mali nyingi kutokana na moto uoiolipuka na kushindwa kuuzima kutokana na ukosefu wa gari hilo.
Chongolo amesema gari Hilo ambalo litakabidhiwa kwenye jeshi la zimamoto na uokoaji wahakikishe lengo la halmashauri linatimia la kuokoa majanga kwa wananchi wa mji wa Tunduma ikiwa ni sambamba na kulitunza vizuri.
"Wafanyabiashara wanatambua Novemba 2011 na Novemba 2021 walivyopata hasara ya bidhaa zao kungua kwa moto ,lakini sasa tunawashukuru halmashauri kununua gari hili ," amesema Chongolo.
Amesema hatutarajii wananchi wanakosa huduma ya gari hili kwa kigezo cha gari bovu, halina maji, halina mafuta hatutaelewana kwani lengo la kuzima majanga ya moto Kwa wananchi yanatatuliwa kwa wakati.
Maiko Mwambene mfanyabiashara katika mji wa Tunduma amesema hatua ya ununuzi wa gari hilo utasaidia kutatua majanga ya moto yanapotokea kwani awali walikuwa wanategemea gari la zimamoto kutoka nchi jirani ya Zambia.
Telezia Mwasa mkazi wa mji wa Tunduma amesema wamepata sana shida juu ya majanga ya moto lakini Kwa sasa itakuwa tofauti miaka ya nyuma kwani maduka mengi yaliungua kutokanana ukosefu wa gari la zimamoto hali iliyokuwa inapelekea kushirikiana na jeshi la polisi kuzima moto kwa njia isiyokuwa rafiki.
Ikumbukwe kuwa mwaka 2011 wafanyabiashara walikubwa na changamoto ya maduka yao kuungua, na mwaka 2021 maduka 43 katika soko la Manzese yaliungua moto, hasara hiyo ilikuwa inatokoea kutokana na ukosefu wa gari la zimamoto na uokoaji.
Mwisho.
0 Comments