TAARIFA KUHUSU MWENENDO WA UHURU WAKUJIELEZA NCHINI KUFUATIA
KUKAMATWA KWA MWANDISHI WA HABARI DINNA MANINGO NA
WANAHARAKATI WENGINE WA KUPIGANIA UHURU WA KUJIELEZA
Ndugu Wananchi na Wapenda Haki ,tunawasalimu !
Ndugu Wananchi,,Hivi karibUuni kumeibuka vitendo vya ukamataji wa wanaharakati mbalimbali
wanaotumia Uhuru na Haki yao ya Kikatiba kutoa taarifa na maoni mbalimbali.Miongoni mwa
wanaharakati ambao hivi karibuni wamekumbana na kadhia hizo ni pamoja na Malisa Godlisten
ambaye mpaka tunaaadaika tamko hili ana kesi Mahakama ya Kisutu Jijijini Dar es Salaam na pia
anakabiliwa na mashitaka matatu mkoani Kilimanajaro yote yakihusiana na Uhuru wa Kujieleza kwa
kutumia mitandao ya kijamii.Mwanaharakati mwingine ni Boniface Jacob ambaye naye anakabiliwa
na mashitaka mawili kwenye Mahakama ya Kisutu Jijini Dares Salaam na wengine ambao
wamekumbwa na ukamataji huu ni pamoja na Mwandishi wa Hbari Dinna Maningo ambaye mpaka
sasa tunapoandika tamko hilo ni siku ya Nne anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kwa
kutuhuma za kuandika habari za tuhuma za ulawiti uliomhusisha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu.
Ndugu Wananchi mbali na matukio hayo ya ukamataji na kufunguliwa kesi wanaharakati
wanaotumia Uhuru wao wa kujileza,pia yapo matukio ya hivi karibuni ya viongozi wa dini pamoja
na wanasiasa mfano Mwenyekiti UVCCM Taifa ambao wametaka Serikali kufungia mitandao ya X
na Istagram kwa kile wanachodai kwamba mitandao hiyo inachochea masuala ya ngono.
Sisi Asasi za Kiraia zinazofanya shughuli za Utetezi wa Haki za Binadamu hususani Haki na Uhuru
wa Kujieleza ( Freedom of Expression) tunaendelea kutoa masikitiko yetu kwa kitendo cha Jeshi la
Polisi Mkoa wa Mwanza kuendelea kumshikilia Mwandishi wa Habari Dina Maningo pasipo kumpa
dhamana wala kumfikisha Mahakama kama sheria inavyoelekeza.na pia tunatoa wito kwa Serikali na
vyombo vingine vya Usalama kuzingatia Katiba ya nchi inayotoa Haki na Uhuru wa Raia wa nchi
kutumia na kufurahia Uhuru na Haki za Kujieleza ambao kwetu wanaharakati wa Haki za Binadamu
ni Haki wezeshi wa HAKI zingine zote
Uhuru wa kujieleza ni Haki iliyo katika Katiba yetu na na Haki za Msingi inayowezesh a Haki zingine
kupatikana ,hivyo vitendo hivi vya Polisi kukamata ,kutisha na kufungulia Waandishi wa
Habari,Wanaharakati mbalimbali nchini havikubaliki na tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi kumwachia
Dina Maningo au wamfikishe Mahakamani .
Mwisho tuwaombe Waandishi wa Habari na Mawakili wajitokeze kupigania haki ya Mwandishi Dina
Maningo pamoja na kupigania haki za wanaharakati wengine Malisa na Boniface na kuendelea
kukemea na kupinga kwa nguvu zote matishio na majaribio ya wanasiasa na wengine wasio na nia
njema na Uhuru wa Kujieleza wanaotaka kuzima na kunyonga Haki na Uhuru huu wa Kujieleza
kwani Shambulio dhidi ya Mwandishi wa Habari ni Shambulio dhidi ya Haki ya Kujieleza na ni
shambulio dhidi ya Haki za Binadamu.
Tamko limetolewa na:
1. CIVIC AND LEGAL AID ORGANIZATION (CILAO)
2. MEDIA DEFENCE INITIATIVE (MDI)
3. OJADACT
4. MAIPAC
5. Foundation for Development Organization - FODEO
0 Comments