Header Ads Widget

UVCCM ILEJE WAHAMASISHANA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Na Moses Ng'wat, Ileje.

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (Uvccm) Wilaya ya Ileje, Mkoani Songwe,  wametakiwa kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu 2024.


Hamasa hiyo imetolewa Juni 19,2024 na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Diana Ngambo, wakati wa kikao cha  baraza la kikanuni la umoja huo kililofanyika katika Ukumbi wa chama hicho uliopo mjini  Itumba wilayani humo.


Ngabo amesema ni wakati wa vijana kujitokeza kugombea nafasi za uongozi kwa lengo la ili kupata watu watakaoendana na kasi ya kusimamia miardi ya maendeleo.


"Tunataka vijana ndio washike nafasi za uongozi na  wazee wetu wabaki kuwa washauri ili tukikosea  waturekebishe, hivyo vijana wenzangu tujitokeze kuomba nafasi muda wa uchukuaji fomu utakapotangazwa na tume ya uchaguzi," amehimiza Ngabo.

Kwa upande wake katibu wa jumuiya hiyo Wilaya, Fatma Mohamed, amewasisitiza vijana hao kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili wawe na sifa ya kupiga kura wakati wa uchaguzi.


"Sifa moja wapo ya kuwa mpiga kura lazima uwe umejiandikisha kwenye daftrai la kudumu ambapo zoezi lake linatarajia kufanyika hivi karibu hivyo mijiandikishe na muwe mabalozi wema kwa wananchi ili wajitokeze," amesema Fatuma.


David Mbughi, katibu wa vijana kata ya Luswisi amesema wanatakiwa kutoogopa kushiriki uchaguzi kwa vitisho kwani wananafasi ya kuwa viongozi bora na wenye nia ya kuleta maendeleo.


Naye, Mjumbe wa baraza la Uvccm wilayani humo, Adamu Myala,  amesema kama vijana wapo tayari kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi ujao kwani vijana wanambio na wazee wabaki washauri.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI