NA AMINA SAIDI,TANGA
Mamlaka ya mapato Tanzania TRA imetoa wito wananchi wote wa Mkoa Tanga kutoa ushirikiano ili kuweza kupata Elimu kwa walipa kodi ambayo hutolewa bure na mamlaka hiyo pamoja na huduma ya TN.
Hayo aliyasema Flavian Byabato ambaye Afìsa mkuu msimamizi wa kodi Tra wakati akizungumza waandishi wa habari katika Banda la TRA kwenye Maonyesho ya Biashara na Utalii ya 11 yaliyofanyika katika viwanja vya shule sekondari Usagara Jijini Tanga.
Aidha alisema kuwa lengo la kuwepo wenye maonyesho ni kuweza kuwapa wafanya biashara waliojitokeza kufanya maonesho hayo kuweza kupata huduma zinazotolewa na TRA ikiwemo ushauri na huduma TN na huduma za kidijitali.
Aliongeza kusema kuwa wanafanya huduma ya TN na makadirio lakini na ushauri juu ya elimu ya digitali kwani maonesho hayo kuna wajasiriamali waliokuja kuonyesha na kuuza bidhaa zao pengine hawajasajiliwa hivyo watapata huduma hiyo.
Byabato alisema pia wanatoa elimu mifumo lakini elimu ya machine ya EFD ili wapate utaratibu upi afuate ili aweze kufuata utaratibu huo.
Mwisho.
0 Comments